Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Nane
Mwenyezi Mungu alisema, Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambao watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu.