Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukombozi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukombozi. Onyesha machapisho yote

12/22/2018

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 3

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 3


Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa.

3/13/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi na Kuingia (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi na Kuingia (6)


Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi.

3/11/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)


Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani.

3/07/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Ishirini na Saba


Mwenyezi Mungu alisema, Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi. Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya wawe mbali nami kila mara, kuwafanya wasitende kulingana na mapenzi Yangu na kuwafanya wapinzani Wangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu? Kila mtu anataka kuishi "kuzimu." Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa maana kila walichohifadhi machoni mwao kinatoka kuzimu. Lakini, binadamu hawana ufahamu wa mambo haya, kwa maana wanasherehekea tu "raha za motoni." Wao huweka mambo haya kama vitu vya thamani karibu nao kwa hofu nyingi kuwa Mimi Nitawapokonya, hivyo kuwaacha bila chanzo cha uhai. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana "hawapendi kujiletea madhara," wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika jamii ili wawe na "maisha ya furaha duniani." Lakini Sitaruhusu mapenzi yao yafanyike, kwa maana lengo Langu haswa ni kuangamiza familia zao. Punde tu Nitakapofika, amani katika jamii zao itatoweka. Nitasambaratisha mataifa yote, na hata familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kujitoa katika minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?

Wanadamu waliutambua upendo Wangu, walinipa huduma itokayo moyoni, na walinitii kwa kweli na kunifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Lakini wanadamu leo hii hawajui kuifikia hali hii ya maisha, bali sasa wanaweza tu kulalamika katika nafsi zao kana kwamba ziliibiwa na mbwa mwitu wakali. Wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, na kunililia wakitaka msaada. Lakini kutoka mwanzo hadi mwisho, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka pale ambapo watu wa kale waliweka ahadi machoni Pangu, walikiri mpaka mwisho wa dunia mbele Zangu, kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo na kigumu kuvumilia. Mara kwa mara, Niliwapa wanadamu msaada kwa sababu ya nia zao. Wanadamu wamekuja mbele Zangu mara nyingi kunitii, na mienendo yao ya kupendeza imekuwa ya kukumbukwa. Mara nyingi wanadamu wamekuja kunionyesha upendo kwa imani isiyotingisika, na hisia zao za kweli zimekuwa za kutamanika. Kwa mara nyingi, wamehatarisha maisha yao ili wanionyeshe upendo, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara tena na tena wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kuna nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama mali Yangu ya thamani, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hivyo ndivyo Nilivyo—mwanadamu hawawezi kutambua kilicho fikirani Mwangu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Hata hivyo, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani aniondoleaye uchungu Ninaohisi? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayeshirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini hakuna hata jambo moja kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, si mambo haya yanatendeka kwa sababu mwanadamu amepotoshwa na adui zake?

Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Ninajawa ghafla na huzuni moyoni Mwangu, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu, siwezi kupata kubadilishana maoni. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Ikawaje hawakuweza kujitoa wenyewe kwa utiifu kwenye njia ya mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakomesha maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni na hasira, Nitashinda ulimwengu wote, bila kumwacha yeyote, na kuwashangaza adui wote. Nataka kuiacha dunia ikiwa kwenye maporomoko, ambamo adui wataishi milele, ili wasiweze kuwapotosha wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeweza kuubadilisha. Ninapoelea ulimwenguni Nikitamba, kila mwanadamu atakuwa na umbo jipya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwandadmu hatalia tena, na hatanililia tena akitaka usaidizi. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

    Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine ya ulimwengu kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao katika hatima yao wenyewe, kwa maana siku yenyewe inakaribia na tarumbeta ya malaika imeshalia tayari. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe kitaanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Litakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki itakapofika ulimwenguni, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi nilipize wanadamu wote na kuamua hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui hata zaidi. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!
Aprili 2,1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

2/17/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi MunguUmuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea.

2/10/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote.

2/09/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.

1/29/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

more
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa na Yohana ilisikika kotekote katika nchi, hivyo ilienea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa Uyahudi, na kila mtu alimwita nabii. Wakati huo, Mfalme Herode alitamani kumuua Yohana, lakini hakuthubutu, kwani watu walimheshimu sana Yohana, na Herode aliogopa kwamba kama angemuua Yohana wangemuasi. Kazi iliyofanywa na Yohana ilikita mizizi miongoni mwa watu wa kawaida, na aliwafanya Wayahudi kuwa waumini.

1/27/2018

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia


Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia


      Biblia imejaa maneno ya Mungu na vile vile uzoefu na ushuhuda kutoka kwa mwanadamu ambao unaweza kutupa uhai na ni yenye manufaa sana kwetu. Bwana Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, bado ataishi: Na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.” (Yohana 11:25-26).

12/18/2017

Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?


Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni?

12/16/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”


Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. 

12/11/2017

Maonyo Matatu | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu

Maonyo Matatu


Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote.

12/01/2017

Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Je, Utatu Mtakatifu Upo?


Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

11/21/2017

Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu


Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika"


Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. 

11/03/2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu


Kristo
Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli


Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe.

11/02/2017

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi


Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.