Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno-Laonekana-msalaba. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno-Laonekana-msalaba. Onyesha machapisho yote

11/02/2017

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi


Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.