Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ufalme. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ufalme. Onyesha machapisho yote

8/20/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Nimeongea hadi kwa kiwango fulani na kufanya kazi hadi kwa kiwango fulani; ninyi nyote mnapaswa kuelewa mapenzi Yangu na kwa viwango tofauti muweze kuzingatia mzigo Wangu. Sasa ndicho kipindi muhimu kutoka katika mwili kuingia katika dunia ya roho, na ninyi ndio watangulizi kwa kutagaa enzi, wanadamu wa ulimwengu wanaovuka miisho ya ulimwengu. Ninyi ni wapendwa Wangu zaidi; ninyi ndio Ninaowapenda. Inaweza kusemwa kwamba Sina wapendwa wengine ila ninyi, kwa sababu jitihada Yangu yote ya bidii imekuwa kwa ajili yenu—inaweza kuwa kwamba hamjui hilo?

7/13/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe. Usidhani kwamba Sitakutelekeza, sasa kwa kuwa una uhakika kunihusu baada ya kuona matendo Yangu—si rahisi hivyo!

6/27/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 84

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 84
Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele. Je, hilo haliko hivyo?

6/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Vipofu! Wajinga! Rundo la takataka lisilo na maana! Nyinyi hutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu! Je, hamfikiri kuwa hii ni dhambi dhidi Yangu? Na zaidi ni kuwa ni kitu ambacho ni vigumu kusamehe! Mungu wa vitendo anakuja miongoni mwenu leo lakini mwajua tu upande Wangu mmoja ambao ni ubinaamu Wangu wa kawaida, na hamjaona kabisa upande Wangu ambao ni wa kiungu kabisa. Je, unafikiri kuwa Sijui anayejaribu kunidanganya kisirisiri?

6/19/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?

5/27/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja”  Sehemu ya Pili

  
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali.

5/19/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 53

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 53

Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Nasema maneno Yangu mbele yenu, na lazima muamini Ninachosema kwa thabiti. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimesema, hakuna neno hata moja limewahi kurudishwa na kila neno litatimizwa. Sasa wakati umewadia na lazima muingie katika uhalisi kwa haraka. Hakuna muda mwingi.

5/11/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 46

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 46

 Yeyote anayejitumia na kujitolea kwa uaminifu kwa ajili Yangu, hakika Nitakukinga mpaka mwisho kabisa; mkono Wangu hakika utakushikilia ili kwamba daima una amani na mwenye furaha daima na kila siku una mwanga Wangu na ufunuo. Hakika Nitakupa baraka Zangu mara dufu, ili uwe na kile Nilicho nacho na umiliki kile Nilicho.

4/22/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu.

12/24/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|3. Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

3. Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Huimin    Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan

Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, na kutotaka kufuata tena, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia. Kwa hiyo kama nilikuwa nikiwatunza waumini wapya au kuongoza wilaya, sikuwahi kufikiri kuwa nilizingatia sana hadhi yangu, kwamba nilikuwa mtu wa aina hiyo.

12/13/2018

"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (1) - Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1)


        Utambulisho

Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

11/01/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Mia Moja na Kumi na Tisa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Mia Moja na Kumi na Tisa


 Ni lazima nyote muelewe nia Zangu, nyote mnapaswa kuelewa hali Yangu ya moyo. Sasa ni wakati wa kujiandaa kurudi Sayuni, sina mawazo ya lolote isipokuwa hili. Mimi Ninatumaini tu kwamba Ninaweza kukutana nanyi siku moja hivi karibuni, na kutumia kila dakika na kila sekunde pamoja nanyi katika Sayuni.

8/24/2018

The Beauty of God’s Kingdom

"Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka katika macho yao; na hakutakuwa na kifo tena, wala uchungu, wala kilio, wala hakutakuwa na maumivu tena; maana ile hali ya kale imepita!"(Ufunuo 21:4)

Mungu, Ufalme, Neema, Kanisa la Mwenyezi Mungu
(Ufunuo 21:3) "Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao."

8/18/2018

Swahili Gospel Choir Song "Ufalme" | New Jerusalem Has Come Down Out of Heaven



Swahili Gospel Choir Song "Ufalme" | New Jerusalem Has Come Down Out of Heaven


Utambulisho

Ufalme, mji wa watakatifu, ufalme wa Kristo.
Katika ufalme, utajiri na utukufu wa Mungu hudhihirishwa.
Umeme unatoka Mashariki na kuangaza hadi Magharibi.
Mwanga wa kweli uko hapa, neno la Mungu limeonekana katika mwili.
Mwokozi amesharudi, akishuka juu ya wingu jeupe.
Watakatifu leo wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi ili kumwabudu Mungu.
Watakatifu wa zamani wamefufuka tena kusimama imara katika siku za mwisho.

4/16/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja

Ni wakati tu ambapo Mungu huanza kunena na kutenda ndipo watu humfahamu Yeye kidogo katika dhana zao. Hapo mwanzo, ufahamu huu huwepo tu ndani ya dhana zao, lakini kadiri muda unavyopita, watu huanza kuhisi kwamba mawazo yao wenyewe yanaendelea kutokuwa na manufaa na hayafai; hivyo, wao huja kuamini yote ambayo Mungu husema, kiasi kwamba wao "hutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya akili zao.” Ni katika akili zao pekee ndipo watu huwa na mahali pa Mungu wa vitendo.

4/13/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 8

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 8

Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni, na huonekana kwamba kutoka kinywani Mwake hutoka mambo yasiyo na kikomo ambayo mwanadamu hayajui, mambo ambayo mwanadamu hawezi kuelewa.

3/20/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tisa

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu.

3/07/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Ishirini na Saba


Mwenyezi Mungu alisema, Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi. Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya wawe mbali nami kila mara, kuwafanya wasitende kulingana na mapenzi Yangu na kuwafanya wapinzani Wangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu? Kila mtu anataka kuishi "kuzimu." Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa maana kila walichohifadhi machoni mwao kinatoka kuzimu. Lakini, binadamu hawana ufahamu wa mambo haya, kwa maana wanasherehekea tu "raha za motoni." Wao huweka mambo haya kama vitu vya thamani karibu nao kwa hofu nyingi kuwa Mimi Nitawapokonya, hivyo kuwaacha bila chanzo cha uhai. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana "hawapendi kujiletea madhara," wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika jamii ili wawe na "maisha ya furaha duniani." Lakini Sitaruhusu mapenzi yao yafanyike, kwa maana lengo Langu haswa ni kuangamiza familia zao. Punde tu Nitakapofika, amani katika jamii zao itatoweka. Nitasambaratisha mataifa yote, na hata familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kujitoa katika minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?

Wanadamu waliutambua upendo Wangu, walinipa huduma itokayo moyoni, na walinitii kwa kweli na kunifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Lakini wanadamu leo hii hawajui kuifikia hali hii ya maisha, bali sasa wanaweza tu kulalamika katika nafsi zao kana kwamba ziliibiwa na mbwa mwitu wakali. Wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, na kunililia wakitaka msaada. Lakini kutoka mwanzo hadi mwisho, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka pale ambapo watu wa kale waliweka ahadi machoni Pangu, walikiri mpaka mwisho wa dunia mbele Zangu, kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo na kigumu kuvumilia. Mara kwa mara, Niliwapa wanadamu msaada kwa sababu ya nia zao. Wanadamu wamekuja mbele Zangu mara nyingi kunitii, na mienendo yao ya kupendeza imekuwa ya kukumbukwa. Mara nyingi wanadamu wamekuja kunionyesha upendo kwa imani isiyotingisika, na hisia zao za kweli zimekuwa za kutamanika. Kwa mara nyingi, wamehatarisha maisha yao ili wanionyeshe upendo, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara tena na tena wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kuna nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama mali Yangu ya thamani, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hivyo ndivyo Nilivyo—mwanadamu hawawezi kutambua kilicho fikirani Mwangu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Hata hivyo, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani aniondoleaye uchungu Ninaohisi? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayeshirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini hakuna hata jambo moja kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, si mambo haya yanatendeka kwa sababu mwanadamu amepotoshwa na adui zake?

Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Ninajawa ghafla na huzuni moyoni Mwangu, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu, siwezi kupata kubadilishana maoni. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Ikawaje hawakuweza kujitoa wenyewe kwa utiifu kwenye njia ya mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakomesha maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni na hasira, Nitashinda ulimwengu wote, bila kumwacha yeyote, na kuwashangaza adui wote. Nataka kuiacha dunia ikiwa kwenye maporomoko, ambamo adui wataishi milele, ili wasiweze kuwapotosha wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeweza kuubadilisha. Ninapoelea ulimwenguni Nikitamba, kila mwanadamu atakuwa na umbo jipya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwandadmu hatalia tena, na hatanililia tena akitaka usaidizi. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

    Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine ya ulimwengu kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao katika hatima yao wenyewe, kwa maana siku yenyewe inakaribia na tarumbeta ya malaika imeshalia tayari. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe kitaanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Litakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki itakapofika ulimwenguni, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi nilipize wanadamu wote na kuamua hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui hata zaidi. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!
Aprili 2,1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

3/05/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni.

3/03/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tatu

Leo si tena Enzi ya Neema, wala enzi ya rehema, bali ni Enzi ya Ufalme ambamo watu wa Mungu wanafichuliwa, enzi ambayo kwayo Mungu hufanya mambo moja kwa moja kwa njia ya uungu. Hivyo, katika kifungu hiki cha maneno ya Mungu, Mungu huongoza wale wote ambao wanayakubali maneno Yake katika ulimwengu wa kiroho.