4/16/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja

Ni wakati tu ambapo Mungu huanza kunena na kutenda ndipo watu humfahamu Yeye kidogo katika dhana zao. Hapo mwanzo, ufahamu huu huwepo tu ndani ya dhana zao, lakini kadiri muda unavyopita, watu huanza kuhisi kwamba mawazo yao wenyewe yanaendelea kutokuwa na manufaa na hayafai; hivyo, wao huja kuamini yote ambayo Mungu husema, kiasi kwamba wao "hutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya akili zao.” Ni katika akili zao pekee ndipo watu huwa na mahali pa Mungu wa vitendo. Kwa kweli, hata hivyo, hawamjui Mungu, na hunena maneno matupu tu. Ilhali ikifananishwa na zamani, wameendelea vizuri mno—ingawa bado wako mbali sana na Mungu Mwenyewe wa vitendo. Kwa nini Mungu husema kila mara, “Kila siku Natembea miongoni mwa mtiririko usiokoma wa watu, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu”? Kadri ambavyo Mungu husema mambo kama hayo, ndivyo watu wanavyoweza kuyafananisha zaidi na Mungu Mwenyewe wa vitendo wa leo, kwa hiyo wanaweza kumjua vizuri zaidi Mungu wa vitendo kwa kweli. Kwa sababu maneno ya Mungu yananenwa kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kutamkwa kwa kutumia lugha ya ubinadamu, watu wanaweza kutambua vyema maneno ya Mungu kwa kuyatathmini dhidi ya vitu yakinifu, na hivyo athari kuu zaidi hutimizwa. Kuongezea, mara kwa mara Mungu hunena kuhusu picha ya "Mimi" ndani ya mioyo ya watu na "Mimi" kwa kweli, ambalo huwafanya watu wawe radhi zaidi kusafisha picha ya Mungu ndani ya mioyo yao, na hivyo kuwa radhi kujua na kufungamana na Mungu Mwenyewe wa vitendo. Hii ni hekima ya maneno ya Mungu. Kadri ambavyo Mungu husema mambo kama hayo, ndivyo faida kwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu huwa kuu zaidi, na hivyo Mungu husema, “Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi kunijua, na hata angekuja kunijua, je, si maarifa kama hayo bado yangekuwa dhana?” Kweli, kama watu wangehitajika kumjua Mungu kufuatana na dhana zao wenyewe, ingekuwa rahisi kwao, wangeburudika na kufurahi, na hivyo Mungu hangekuwa dhahiri daima, na asiye wa vitendo katika mioyo ya watu, ambalo lingethibitisha kwamba Shetani, na si Mungu, anashikilia utawala juu ya ulimwengu wote; hivyo, maneno ya Mungu kwamba "Nimerejesha mamlaka Yangu" yangesalia matupu daima.
Mbona Mungu husema kila mara kwamba "Mambo yote yanakimya" Yawezekana kwamba mambo yote yanasimama kabisa? Yawezekana kwamba milima mikubwa inakimya kwa kweli? Kwa hiyo mbona watu hawana ufahamu wa hili? Yawezekana kwamba neno la Mungu lina makosa? Au Mungu anatia chumvi? Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu hufanya hutekelezwa katika mazingira fulani, hakuna ambaye hukifahamu, au ambaye ana uwezo wa kukiona kwa macho yake mwenyewe, na yote ambayo watu wanaweza kufanya tu ni kumsikiliza Mungu akinena. Kwa sababu ya uadhama ambao Mungu hutenda, wakati ambapo Mungu hufika, ni kana kwamba kumekuwa na mabadiliko makubwa mno mbinguni na duniani; na kwa Mungu, huonekana kwamba wote wanatazama wakati huu. Leo, ukweli bado haujafika. Watu wamejifunza kidogo tu kutoka kwa sehemu ya maana halisi ya maneno ya Mungu. Maana ya kweli inangoja wakati ambao watajisafisha na dhana zao; wakati huo tu ndipo watakuwa na fahamu ya kile ambacho Mungu mwenye mwili anafanya duniani na mbinguni leo. Ndani ya watu wa Mungu Uchina hakuna tu sumu ya joka kubwa jekundu. Hiyo, pia, ndiyo asili ya joka kubwa jekundu iliyofichuliwa kwa wingi zaidi, na kwa dhahiri zaidi, ndani yao. Lakini Mungu hazungumzi kuhusu hili moja kwa moja, Akitaja tu kidogo kuhusu sumu ya joka kubwa jekundu. Kwa njia hii, Hayafichui makovu ya mwanadamu moja kwa moja, ambalo ni la manufaa zaidi kwa maendeleo ya mwanadamu. Watoto wa joka kubwa jekundu hawapendi kuitwa ukoo wa joka kubwa jekundu mbele ya wengine. Ni kana kwamba maneno “joka kubwa jekundu” huleta aibu kwao; hakuna yeyote kati yao aliye radhi kuzungumza kuhusu maneno haya, na hivyo Mungu husema tu, “hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina.” Kwa usahihi zaidi, Mungu amekuja hasa kuwashinda wawakilishi wa kiumboasili wa watoto wa joka kubwa jekundu, ambalo ni umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu Uchina.

“Nijapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza kazi ya uchungaji wakati huo huo.” Kwa kweli, haichukuliwi neno kwa neno kwamba Roho wa Mungu huwasili tu katika ulimwengu wa mwanadamu wakati ambapo malaika huanza kazi yao miongoni mwa watu wote. Badala yake, sehemu hizi mbili za kazi—kazi ya uungu na uchungaji wa malaika—hutekelezwa sawia. Linalofuata, Mungu huzungumza kidogo kuhusu uchungaji wa malaika. Wakati ambapo Yeye husema kwamba “wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao wenyewe, tukio la kila aina za maono,” watu wengi sana huwa na mawazo tele kuhusu neno "maono." Maono yanahusu matukio ya rohoni katika mawazo ya watu. Lakini yaliyomo katika kazi husalia ufahamu wa Mungu Mwenyewe wa vitendo. Maono ni njia ambayo kwayo malaika hufanya kazi. Yanaweza kuwapa watu hisia au ndoto, yakiwakubalia kutambua kuweko kwa malaika. Lakini malaika husalia wasioonekana kwa mwanadamu. Mbinu ambayo kwayo wao hufanya kazi miongoni mwa wana na watu wa Mungu ni kuwapa nuru na kuwaangaza moja kwa moja, kuongezea kwayo ni kuwashughulikia na kuwavunja. Wao hutoa mahubiri mara chache. Kwa kawaida, mawasiliano kati ya watu ni jambo la pekee; hili ndilo linalofanyika katika mataifa nje ya Uchina. Ndani ya maneno ya Mungu kuna ufunuo wa hali za kuishi za wanadamu wote—kwa kawaida, hili linaelekezwa hasa kwa watoto wa joka kubwa jekundu. Kati ya hali mbalimbali za kiroho za wanadamu wote, Mungu huteua zile ambazo ni za uwakilishi ili zitumike kama mifano. Hivyo, maneno ya Mungu huwavua watu wakawa uchi, na hawaoni aibu yoyote, ama sivyo hawana muda wa kujificha kutoka kwa nuru iangazayo, na wao hushindwa katika ujanja wao. Tabia nyingi za mwanadamu ni picha nyingi kupita kiasi, ambazo Mungu amechora kutoka nyakati za kale mpaka leo, na ambazo Atachora kutoka leo mpaka kesho. Yote ambayo Yeye huchora ni ubaya wa mwanadamu: Wengine hutokwa na machozi gizani, inavyoonekana kwa nje wao husikitishwa kwa ajili ya kutoona tena, wengine hucheka, wengine hupigwa kwa nguvu na mawimbi makubwa, wengine hutembea juu ya barabara za mlima zinazoinuka na kushuka, wengine hutafuta katikati ya nyika kubwa mno, wakitetemeka kwa woga, kama ndege aliyegutushwa na mlio tu wa uzi wa uta, wakitishwa kabisa na kuliwa na wanyama wa mwitu katika milima. Mikononi mwa Mungu, hizi tabia nyingi mbaya hugeuka kuwa za kugusa, uwakilishaji wa picha kama za maisha, nyingi ya hizo za kutisha sana kutazama, la sivyo za kiasi cha kutosha kuwaogofya watu na kuwaacha waliokanganyikiwa na kutatanishwa. Machoni pa Mungu, vyote vinavyoonyeshwa ndani ya mwanadamu ni ubaya tu, na hata ingawa kinaweza kuchochea huruma, bado ni ubaya. Sehemu maalum ya tofauti kati ya mwanadamu na Mungu ni kwamba udhaifu wa mwanadamu upo katika mwelekeo wake wa kuonyesha ukarimu wake kuelekea wengine. Mungu, hata hivyo, Amekuwa yule yule kila mara kwa mwanadamu, ambalo lina maana kwamba Yeye kila mara Amekuwa na mtazamo ule ule. Yeye kila mara si mkarimu jinsi watu hufikiria, kama mama mwenye tajiriba ambaye watoto wake kila mara huwa katika sehemu ya mbele kabisa ya mawazo yake. Kwa kweli, kama Mungu hangetaka kutumia mbinu nyingi ili kulishinda joka kubwa jekundu, hakuna vile ambavyo Angejisalimisha kwa aibu kama hiyo, Akijiruhusu kutiishwa chini ya udhaifu wa mwanadamu. Kufuatana na asili ya Mungu, yote ambayo watu hufanya na kusema huchochea ghadhabu ya Mungu, na wao wanapaswa kuadibiwa. Machoni pa Mungu, hakuna yeyote kati yao anayefikia kiwango, na kila mmoja wao ni shabaha ya mashambulio ya Mungu. Kwa sababu ya kanuni za kazi ya Mungu Uchina, na, zaidi ya hayo, kwa sababu ya asili ya joka kubwa jekundu, kuongeza kwa hilo ni ukweli kwamba Uchina ni taifa la joka kubwa jekundu, na nchi ambayo kwayo Mungu mwenye mwili huishi, Mungu lazima amezee hasira Yake na kuwashinda watoto wote wa joka kubwa jekundu; ilhali Yeye kila mara Atawachukia sana watoto wa joka kubwa jekundu, yaani, Yeye kila mara Atayachukia sana yote ambayo hutoka kwa joka kubwa jekundu—na hili halitabadilika kamwe.
Hakuna ambaye amewahi kufahamu matendo yoyote ya Mungu, wala matendo Yake hayajawahi kutazamwa na chochote. Wakati ambapo Mungu alirudi Sayuni, kwa mfano, ni nani aliyefahamu hili? Hivyo, maneno kama “Naja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna yeyote aliyewahi kuniona?” yanaonyesha kwamba mwanadamu kweli hukosa welekevu wa kukubali matukio ya ufalme wa kiroho. Zamani, Mungu alisema kwamba "jua ni la joto, mwezi ni wa mng'aro" wakati wa kurudi Kwake Sayuni. Kwa sababu watu bado wameshughulishwa na kurudi kwa Mungu Zayuni—kwa sababu bado hawajaliacha—Mungu hutamka moja kwa moja maneno "jua ni la joto, na mwezi ni wa mng'aro" ili kupatana na dhana za watu. Kutokana na hilo, wakati ambapo dhana za watu hugongwa na maneno ya Mungu, wao huona kwamba matendo ya Mungu ni ya ajabu sana, na huona kwamba maneno Yake ni ya maana sana na yasiyoweza kuelewaka, na yasiyotambulikana kwa wote; hivyo, wao huliweka jambo hili pembeni kabisa, na kuhisi ubayana kidogo ndani ya roho zao, kana kwamba Mungu amerudi Sayuni tayari, na kwa hiyo watu hawazingatii sana jambo hili. Kuanzia wakati huo kuendelea, wao hukubali maneno ya Mungu kwa moyo mmoja na fikira moja, na hawawi na wasiwasi tena kwamba watafikwa na msiba mkuu baada ya kurudi kwa Mungu Sayuni. Ni wakati huo tu ndiyo huwa rahisi kwa watu kuyakubali maneno ya Mungu, kulenga zingatio lao lote kwa maneno ya Mungu, wakiachwa bila hamu ya kufikiria jambo lingine lolote.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni