Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Ishirini na Saba
Mwenyezi Mungu alisema, Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi. Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya wawe mbali nami kila mara, kuwafanya wasitende kulingana na mapenzi Yangu na kuwafanya wapinzani Wangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu? Kila mtu anataka kuishi "kuzimu." Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa maana kila walichohifadhi machoni mwao kinatoka kuzimu. Lakini, binadamu hawana ufahamu wa mambo haya, kwa maana wanasherehekea tu "raha za motoni." Wao huweka mambo haya kama vitu vya thamani karibu nao kwa hofu nyingi kuwa Mimi Nitawapokonya, hivyo kuwaacha bila chanzo cha uhai. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana "hawapendi kujiletea madhara," wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika jamii ili wawe na "maisha ya furaha duniani." Lakini Sitaruhusu mapenzi yao yafanyike, kwa maana lengo Langu haswa ni kuangamiza familia zao. Punde tu Nitakapofika, amani katika jamii zao itatoweka. Nitasambaratisha mataifa yote, na hata familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kujitoa katika minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?
Wanadamu waliutambua upendo Wangu, walinipa huduma itokayo moyoni, na walinitii kwa kweli na kunifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Lakini wanadamu leo hii hawajui kuifikia hali hii ya maisha, bali sasa wanaweza tu kulalamika katika nafsi zao kana kwamba ziliibiwa na mbwa mwitu wakali. Wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, na kunililia wakitaka msaada. Lakini kutoka mwanzo hadi mwisho, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka pale ambapo watu wa kale waliweka ahadi machoni Pangu, walikiri mpaka mwisho wa dunia mbele Zangu, kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo na kigumu kuvumilia. Mara kwa mara, Niliwapa wanadamu msaada kwa sababu ya nia zao. Wanadamu wamekuja mbele Zangu mara nyingi kunitii, na mienendo yao ya kupendeza imekuwa ya kukumbukwa. Mara nyingi wanadamu wamekuja kunionyesha upendo kwa imani isiyotingisika, na hisia zao za kweli zimekuwa za kutamanika. Kwa mara nyingi, wamehatarisha maisha yao ili wanionyeshe upendo, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara tena na tena wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kuna nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama mali Yangu ya thamani, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hivyo ndivyo Nilivyo—mwanadamu hawawezi kutambua kilicho fikirani Mwangu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Hata hivyo, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani aniondoleaye uchungu Ninaohisi? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayeshirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini hakuna hata jambo moja kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, si mambo haya yanatendeka kwa sababu mwanadamu amepotoshwa na adui zake?
Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Ninajawa ghafla na huzuni moyoni Mwangu, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu, siwezi kupata kubadilishana maoni. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Ikawaje hawakuweza kujitoa wenyewe kwa utiifu kwenye njia ya mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakomesha maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni na hasira, Nitashinda ulimwengu wote, bila kumwacha yeyote, na kuwashangaza adui wote. Nataka kuiacha dunia ikiwa kwenye maporomoko, ambamo adui wataishi milele, ili wasiweze kuwapotosha wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeweza kuubadilisha. Ninapoelea ulimwenguni Nikitamba, kila mwanadamu atakuwa na umbo jipya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwandadmu hatalia tena, na hatanililia tena akitaka usaidizi. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …
Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine ya ulimwengu kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao katika hatima yao wenyewe, kwa maana siku yenyewe inakaribia na tarumbeta ya malaika imeshalia tayari. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe kitaanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Litakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki itakapofika ulimwenguni, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi nilipize wanadamu wote na kuamua hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui hata zaidi. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!

Aprili 2,1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni