9/04/2018

Enzi ya Sheria: Yaliyomo na Matokeo ya Kazi ya Mungu

Enzi ya Sheria: Yaliyomo na Matokeo ya Kazi ya Mungu


“wakati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilifaa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kuunda madhabahu, namna ya kuyaunda madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kuamuru namna ambavyo binadamu alifaa kuishi—kile alichofaa kutilia maanani katika maisha, kile alichofaa kutii, kile anachofaa na hafai kufanya. Kile Mungu alichoweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinakubalika chote, na pamoja na tamaduni, taratibu, na kanuni hizi Aliwastanisha tabia ya watu, kuongoza maisha yao, kuongoza uanzishaji wao wa sheria za Mungu, kuwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, kuwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa mambo mengine yote ambayo Mungu alikuwa amemuumbia binadamu na yaliyomilikiwa na mpangilio na marudio ya mara kwa mara na ya kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi kuweka vipimo kwa binadamu, ili hapa duniani binadamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. ”
kutoka kwa Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kazi ya Mungu, Umeme wa Mashariki“Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. Yehova Aliwakabidhi sheria hizi wana wa Israeli ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Wamisri, na zilinuiwa kuwazuia wana wa Israeli, na ndiyo yaliyokuwa mahitaji Yake kwao. Kama mtu alitii sheria ya Sabato, kama mtu aliheshimu wazazi wake, kama mtu aliabudu miungu na kadhalika, hizi ndizo zilizokuwa kanuni ambazo mtu alihukumiwa na kujulikana kama mwenye dhambi au mwenye haki. Kama mtu alichomwa na moto wa Yehova, au kupigwa na mawe hadi kufa, au kupokea baraka za Yehova, vyote hivi viliamuliwa kulingana na kama mtu alitii sheria hizi. Wale ambao hawakutilia maanani Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakutilia maanani Sabato wangeteketezwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuheshimu wazazi wao wangepigwa mawe pia hadi kufa. Haya yote yalishauriwa na Yehova. Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria. Ingawaje Yehova Aliongea sana na Alifanya kazi nyingi, Aliwaongoza tu kwa njia nzuri huku Akiwafunza watu hawa wasiojua namna ya kuwa na wema, namna ya kuishi, namna ya kuelewa njia ya Yehova. Katika sehemu kubwa ya kazi Yake kwa hakika Alinuia kuruhusu watu Wake kufuatilia njia Yake na kufuata sheria Yake. Kazi ilifanyiwa watu ambao walikuwa wamepotoka kidogo; haikujali sana mageuzi ya tabia au ukuzi wa maisha. Alijali tu matumizi ya sheria ya kuzuia na kudhibiti watu. Kwa wana wa Israeli wakati huo, Yehova Alikuwa tu Mungu kwenye hekalu, Mungu kwenye mbingu. Alikuwa mnara wa wingu, mnara wa moto. Kile ambacho Yehova Aliwahitaji kufanya kilikuwa ni kutii kile ambacho watu wanajua leo kama sheria na mafundisho Yake—mtu angeweza hata kusema taratibu—kwa sababu kazi ya Yehova haikunuiwa kuwabadilisha, lakini kuwapatia vitu vingi ambavyo binadamu anastahili kuwa navyo, kuwaambia kutoka kwenye kinywa Chake mwenyewe, kwa sababu baada ya binadamu kuumbwa, binadamu hakujua chochote kuhusu kile alichostahili kumiliki. Na kwa hivyo Yehova Aliwapatia vitu walivyostahili kumiliki katika maisha yao hapa ulimwenguni, Akawafanya watu Aliokuwa Amewaongoza kuzidi vizazi vyao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova Alichowapatia kilizidi kile Alichokuwa Amepatia Adamu na Hawa hapo mwanzo. Licha ya hayo yote, kazi ambayo Yehova Alifanya Israeli ilikuwa tu kuongoza binadamu na kuwafanya kutambua Mungu wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, Aliwaongoza tu. Hii ndiyo jumla ya kazi ya Yehova kwenye Enzi ya Sheria. Ndiyo maelezo ya ziada, hadithi ya kweli, kiini cha kazi Yake kwenye nchi nzima ya Israeli na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—katika kudhibiti mwanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na haya yote kazi nyingi zaidi ilijitokeza kwenye mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.”
kutoka kwa Kazi Katika Enzi ya Sheria


Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kujua Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni