5/22/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 55

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 55

Mwenyezi Mungu anasema: Ubinadamu wa kawaida ambao huzungumziwa si wa mwujiza sana kama watu wanavyofikiria, lakini unaweza kuvuka mipaka ya mafungo ya watu wote, matukio, na vitu, kupita mipaka ya nguvu za mazingira, na unaweza kunikaribia Mimi na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mahali popote na katika mazingira yoyote. Ninyi daima hutafsiri vibaya nia Zangu. Ninaposema mnapaswa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, mnajizuia na kudhibiti miili yenu.  Lakini huzingatii kutafuta kwa makini ndani ya roho, ila kwa kile mnachovaa kwa nje pekee, ukikosa kuangalia ufunuo Wangu ndani yako, na kuhimiza Kwangu ndani yako. Jinsi ulivyo mzembe! Mzembe sana! Inaweza kuwa kwamba kumaliza kile ambacho Nimekuaminia ni ufanisi mkubwa? Wewe ni mpumbavu! Huzingatii kukita mizizi kwa kina! "Usiwe jani kwa mti, ila uwe mzizi wa mti huo"—huo kweli ni wito wako? Hujali! Mzembe! Unaridhika unapofikiria kuwa una kitu kidogo. Jinsi unavyojali mapenzi Yangu kidogo sana! Kuanzia sasa kuendelea jihadhari. Usiwe baridi. Usiwe hasi! Unapohudumu, Nikaribie mara kwa mara na kuwasiliana kwa karibu na Mimi. Hii ndiyo njia yako ya pekee. Najua kwamba tayari umejinyima, unajua upungufu wako mwenyewe, unajua udhaifu wako mwenyewe. Lakini kujua tu hakutoshi. Unahitaji kushirikiana na Mimi na punde unapoelewa nia Zangu ziweke katika vitendo mara moja. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kuonyesha kujali mzigo Wangu, njia bora kabisa ya kutii.

Bila kujali jinsi unavyonitendea, Nataka kutekeleza mapenzi Yangu kwako na watakatifu wote, na Nataka mapenzi Yangu yatekelezwe bila kuzuiwa katika nchi yote. Tambua hili kikamilifu! Hili linahusu amri Zangu za utawala! Huogopi hata kidogo? Hutetemeki kwa hofu kwa sababu ya vitendo vyako na mienendo yako? Miongoni mwa watakatifu wote karibu wote hawahisi nia Yangu. Hutaki kuwa wa kipekee kama mtu anayefikiria mapenzi Yangu kabisa? Je, wajua? Nia yangu ya dharura kwa sasa ni kutafuta kundi la watu wanaoweza kufikiria mapenzi Yangu kabisa. Hutaki kuwa mmoja wao? Hutaki kujitumia kwa ajili Yangu, kujitolea kwa ajili Yangu? Hutaki kulipa gharama hata kidogo, kutoa juhudi hata kidogo! Mambo yakiendelea kuwa hivyo, juhudi Yangu ya bidii itakuwa bure kwenu. Baada ya Mimi kukuonyesha hilo, bado hujaelewa uzito wa suala hili?
"Kwa wale ambao kweli wanatumia rasilmali kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki pakubwa." Unaona! Nimekuambia hili mara kadhaa, lakini bado una mashaka mengi, ukiogopa mazingira ya jamii, ukiogopa mazingira ya nje. Kweli hujui kinachokufaa! Nawatumia tu watu waaminifu, wa kawaida, na wazi. Umekuwa na furaha na radhi kwa Mimi kukutumia, lakini kwa nini bado una wasiwasi sana? Inaweza kuwa kwamba maneno Yangu hayana athari hata kidogo kwako? Nimesema kuwa Nakutumia wewe, ilhali huwezi kuamini hilo kwa uthabiti. Kila mara unashuku, ukiogopa kwamba Nitakuacha. Dhana zako zimefungwa sana! Ninaposema kwamba Nakutumia hilo linamaanisha Nakutumia. Kwa nini una shaka sana kila mara? Je, ni kwamba Sijaongea kwa wazi vya kutosha? Kila neno ambalo Nimesema ni kweli. Hakuna tamko hata moja ambalo si la kweli. Mwanangu! Niamini. Jitolee nafsi kwa niaba Yangu, na hakika Nitajitolea nafsi kwako!

Chanzo: Maneno ya Mungu | Sura ya 55
Wasiliana Nasi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni