"Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka katika macho yao; na hakutakuwa na kifo tena, wala uchungu, wala kilio, wala hakutakuwa na maumivu tena; maana ile hali ya kale imepita!"(Ufunuo 21:4)
(Ufunuo 21:3) "Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao."
Mungu alisema, "Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee, na hakuna mtu yuko alivyokuwa. Ninapumzika katika enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima, na Nimeridhika kikamilifu, kwani kila kitu kimerejesha utakatifu wake, na Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena, na watu duniani wanaweza kuishi maisha tulivu na ya kuridhisha chini ya mwongozo Wangu. Watu wote wanasimamia kila kitu mkononi Mwangu, watu wote wamerejesha akili yao ya awali na mwonekano wao wa kiasili; hawafunikwi tena na vumbi, lakini, ndani ya ufalme Wangu, ni wasafi kama lulu, kila mmoja akiwa na uso kama wa mtakatifu ndani ya moyo wa binadamu, kwani ufalme Wangu umekuwa imara miongoni mwa binadamu."
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
"Kotekote ulimwenguni, Mungu na mwanadamu ndio pekee wanaoishi. Hakuna vumbi wala uchafu, na vitu vyote vinafanywa upya, kama mwanakondoo mdogo anayelala katika ukanda wa mbuga wa kijani kibichi chini ya anga, akifurahia neema yote ya Mungu. Na ni kwa sababu ya ujio wa kijani kibichi hiki ndiposa pumzi ya uhai inaangaza, kwani Mungu anakuja duniani kuishi pamoja na mwanadamu milele yote, kama ilivyosemwa kutoka kinywani mwa Mungu kwamba “Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena.” Hii ni ishara ya kushindwa kwa shetani, ni siku ya pumziko la Mungu, na siku hii itatukuzwa na kutangazwa na watu wote, na itafanyiwa kumbukumbu na watu wote. Wakati ambapo Mungu ametulia juu ya kiti cha enzi pia ndio wakati ambapo Mungu anahitimisha kazi Yake duniani, na ndio wakati ule ambao siri zote za Mungu zinaonyeshwa kwa mwanadamu; Mungu na mwanadamu watakuwa katika upatanifu daima, hawatakuwa mbali tena—haya ni mandhari mazuri ya ufalme!"
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kujua Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni