Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

7/24/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 96

Maneno ya Mungu | Sura ya 96

Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. 

7/07/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu?

6/29/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole, wanaokuwa na uhakika kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).

6/25/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 82

Matamshi ya Mungu | Sura ya 82

Wote wanaogopa wanaposikia neno Langu. Wote wamejawa na hofu. Mnaogopa nini? Sitawaua! Ni kwa sababu mnahisi hatia na mnaogopa kugunduliwa. Yale unayoyafanya nyuma Yangu ni ya upuuzi na yasiyo na maana kabisa. Hili limenifanya Nikuchukie sana hivi kwamba Ninatamani sana Ningekuwa nimewatupa wale ambao Sikuwa nimewajaalia wala kuwachagua katika shimo lisilokuwa na mwisho wavunjwe vipande vipande. Hata hivyo, Nina mpango Wangu, Nina malengo Yangu.

6/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Vipofu! Wajinga! Rundo la takataka lisilo na maana! Nyinyi hutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu! Je, hamfikiri kuwa hii ni dhambi dhidi Yangu? Na zaidi ni kuwa ni kitu ambacho ni vigumu kusamehe! Mungu wa vitendo anakuja miongoni mwenu leo lakini mwajua tu upande Wangu mmoja ambao ni ubinaamu Wangu wa kawaida, na hamjaona kabisa upande Wangu ambao ni wa kiungu kabisa. Je, unafikiri kuwa Sijui anayejaribu kunidanganya kisirisiri?

6/19/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?

6/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi Yangu yote ni maonyesho ya mapenzi Yangu. Ni nani anayeweza kuudhukuru mzigo Wangu? Nani anayeweza kuelewa nia Yangu? Je, mmefikiria kila moja ya maswali Niliyoibua kwenu? Uzembe ulioje! Unathubutu vipi kuvuruga mipango Yangu? Wewe u mshenzi kweli! Kazi kama hii ya pepo wabaya ikiendelea, Nitawatupa mautini mara moja katika shimo lisilo na mwisho! Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya.

6/11/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Sharti unitegemee kuondoa upungufu ama udhaifu mara tu unapougundua. Usichelewe; vinginevyo kazi ya Roho Mtakatifu atakuwa mbali sana nawe, na utaanguka nyuma mbali sana. Kazi ambayo Nimekuaminia inaweza kutimizwa kwa kupitia tu kukaribia kwako mara kwa mara, kuomba, na kuwa na ushirika katika uwepo Wangu. Kama sivyo, hakuna matokeo yoyote yatakayofikiwa, na kila kitu kitakuwa bure. Kazi Yangu leo si kama ilivyokuwa awali. Kadiri ya maisha kwa watu Ninaowapenda si kama ilivyokuwa mbeleni.

6/04/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 66

Sauti ya Mungu | Sura ya 66

Kazi Yangu imeendelea hadi hatua ya sasa na yote imefuata mipango ya busara ya mkono Wangu, na pia kuwa fanikio Langu kuu. Nani kati ya wanadamu anaweza kufanya kitu kama hiki? Na je, si wanaona ni afadhali waingilie kati usimamizi Wangu? Lakini lazima ujue kuwa hakuna namna yeyote anaweza kufanya kazi Yangu badala Yangu, sembuse kuizuia, kwani hakuna yeyote anayeweza kusema au kufanya vitu Nifanyavyo na kusema. 

6/03/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 65


Sauti ya Mungu | Sura ya 65
Maneno Yangu daima yanaendeleza barabara, yaani yanaonyesha udhaifu wenu wa jaala, vinginevyo bado mgekuwa mnakokota visigino vyenyu, bila wazo la muda gani ulioko sasa. Fahamu hili! Mimi Hutumia njia ya upendo ili kuwaokoa. Bila kujali jinsi nyinyi mlivyo, bila shaka Nitakamilisha mambo ambayo Nimekubali bila kufanya kosa lolote. Je, Ninaweza, Mwenyezi Mungu Mwenye haki, kufanya kosa? Je, hiyo siyo dhana ya mtu? Niambieni, kila kitu Mimi Hufanya na kusema si kwa ajili yenu?

5/24/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 57

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 57

Je, umechunguza kila fikira na mawazo yako, na kila tendo lako? Uko wazi kuhusu gani kati ya haya yanalingana na mapenzi Yangu na gani hayalingani? Huna uwezo wa kutambua haya! Mbona hujaja mbele Yangu? Je, ni kwa sababu Sitakuambia, au ni kwa ajili ya sababu nyingine? Unapaswa kujua hili! Kujua kwamba wale walio wazembe hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu kabisa au kupokea mwangaza na ufunuo mkuu.

5/03/2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

4/26/2019

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea.

4/25/2019

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

    Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au ndugu wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali kwa mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu.

4/24/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu

Katika uzoefu wote wa Petro, alikumbana na mamia ya majaribio. Ingawa watu wa leo wanafahamu neno “jaribio,” wao huchanganyikiwa kuhusiana na maana yake ya kweli na hali. Mungu hutuliza azimio la watu, husafisha imani yao, na hukamilisha kila sehemu yao—na hii hufanikishwa kimsingi kupitia majaribio, ambayo pia ni kazi ya Roho Mtakatifu iliyofichwa. Inaonekana kama kwamba Mungu amewaacha watu, na kwa hivyo wasipokuwa waangalifu, watayaona majaribio haya kama majaribu ya Shetani.

4/23/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi MunguFumbo la Kupata Mwili (4)

Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Ikiwa ungewaelezea, mambo haya ya kiini, wasingekuwa tena wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia na wewe. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu.

1/26/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14


Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo.

12/23/2018

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 4

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 4


Daima tutakuwa tukiangalia na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteka kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji ambayo huondoa kiu kutoka kwa roho zetu zilizokauka. Ni lazima tuwe tayari wakati wowote, kujitakasa kutokana na haki ya kibinafsi, kiburi chetu, kujiridhisha kibinafsi, na ridhaa yetu, kila moja kuzaliwa kutoka kwa tabia yetu ya kishetani.