Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuijua-Sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuijua-Sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

10/01/2019

Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili



"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili


Mwenyezi Mungu anasema, “Maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia, na upanga mkali ukatao kuwili, ambao unaweza kumshinda Shetani” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ni kama upanga wenye makali pande mbili, yanayoweza kushinda nguvu zote za uovu. Je, umepitia nguvu na mamlaka ya kutisha ya maneno ya Mungu?

Tazama Zaidi: Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"

9/28/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 111


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 111


Mataifa yote yatabarikiwa kwa sababu Yako; watu wote watanikaribisha kwa shangwe na kunisifu kwa sababu Yako. Ufalme Wangu utafanikiwa na kukua, na utabaki milele. Hakuna mtu ataruhusiwa kuukanyaga na hakuna kitu kitaruhusiwa kuwepo ambacho hakikubaliani na Mimi, kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye uadhama na asiyekosewa Mwenyewe. Sikubali mtu yeyote anihukumu na Sikubali mtu yeyote kutolingana na Mimi. Hili linatosha kuonyesha tabia Yangu na uadhama Wangu.

9/25/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 110

Sauti ya Mungu | Sura ya 110


Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.

9/22/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 109


Maneno ya Mungu | Sura ya 109


Ninatoa matamko kila siku, kuzungumza kila siku, na kufichua ishara Zangu kuu na shani kila siku. Haya yote ni kazi ya Roho Wangu. Machoni pa watu Mimi ni mwanadamu tu, lakini hasa ni katika mwanadamu huyu ndipo Ninafichua vyote Vyangu na nguvu Yangu kuu.

Kwa kuwa watu humpuuza mwanadamu Niliye na huyapuuza matendo Yangu, wanafikiri kuwa hivi ni vitu ambavyo hufanywa na wanadamu. Lakini mbona hufikiri: Je, watu wanaweza kutimiza yale Ninayoyatenda? 

9/10/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107


Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.) Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi.

9/07/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 106

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 106


Wale wasioyajua maneno Yangu, wale wasioujua ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale wanaokataa uungu Wangu wote wataangamizwa hadi wasikuwepo. Hakuna atakayeachiliwa kutokana na hili, na wote lazima wapitie hili kwa sababu ni amri Yangu ya utawala, na ndicho kifungu kikali zaidi cha amri Yangu. Wale wasioyajua maneno Yangu ni wale ambao wamesikiliza yale ambayo Nimesema wazi, ilhali bado hawayajui, kwa maneno mengine wale ambao hawaelewi masuala ya kiroho (kwa kuwa Sijaumba sehemu hii ya mwili kwa ajili ya wanadamu, Sihitaji mengi kutoka kwao; Nahitaji tu kwamba wasikilize maneno Yangu na kisha wayaweke katika matendo).

9/01/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 104

Sauti ya Mungu | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme.

8/17/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 101

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Sauti ya Mungu | Sura ya 101

Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka Kwangu, au hutoka kwa Shetani? 

8/14/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 100

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 100

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote. 

7/07/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu?

7/06/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu  | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

6/26/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 83

Maneno ya Mungu | Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni ni? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani ameipotosha sana, ni kina nani wachache ambao wako jinsi Nipendavyo?

6/24/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 81

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 81

Oh, enzi hii mbaya na yenye uzinzi! Nitakumeza! Mlima Sayuni! Simama unisifu Mimi! Kwa kukamilika kwa mpango Wangu wa usimamizi, kwa kukamilika kwa kazi Yangu kuu, ni nani athubutuye kutoinuka na kufurahi! Ni nani athubutuye kutoinuka na kuruka kwa furaha bila kukoma! Atakutana na kifo chake mkononi Mwangu. Mimi hutekeleza haki kwa kila mtu, bila huruma hata kidogo au upendo wa fadhila, na bila kupendelea. Watu wote! Simameni ili kutoa sifa, Nipeni utukufu!

6/23/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani.

9/15/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Dibaji

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Dibaji


Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. 

9/09/2017

Sauti ya Mungu | Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki 

Sauti ya Mungu | Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya


Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya.