Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Usomaji. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Usomaji. Onyesha machapisho yote

12/06/2019

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.”

Iliyotazamwa Mara Nyingi:

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani" ( Filamu za Injili )


11/22/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"



Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho."

11/21/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”



Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. ... Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.”

10/28/2019

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"


Mwenyezi Mungu anasema, "Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno 'mpya' na 'ajabu.' 'Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu'; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu."

9/27/2018

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki



Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Utambulisho

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

8/27/2018

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Roho Mtakatifu, Mungu wa Vitendo, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki




Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe


Utambulisho

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo.