Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mkate-wa-kila-Siku. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mkate-wa-kila-Siku. Onyesha machapisho yote

12/15/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

 

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.


12/13/2019

Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

 


       Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.

12/06/2019

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.”

Iliyotazamwa Mara Nyingi:

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani" ( Filamu za Injili )


11/04/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili



Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia.”
Video Husika:

     Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu