Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85
Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole, wanaokuwa na uhakika kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).
Yeyote Nimchukiaye (hiki ni kitu kilicho ndani Yangu ambacho watu hawawezi kukijua kutoka nje) ni mtu ambaye kwa hakika atapitia laana Zangu, na ni wale ambao bila shaka ni miongoni mwa watoto wa joka kuu jekundu, hivyo watashiriki katika laana Yangu ya joka kuu jekundu. Kwa wale ambao Siwezi kuwatazama, ambao ubora wao una upungufu na wasioweza kukamilishwa au kutumiwa na Mimi, bado watakuwa na nafasi ya kuokolewa na watakuwa wale miongoni mwa wana Wangu. Iwapo mtu huyu hana ubora wowote Wangu, hawezi kuyaelewa mambo ya kiroho wala kunijua Mimi, lakini ana moyo ulio na shauku, basi atateuliwa kama mmoja wa watu Wangu. Ninawadhukuru wale wanaoshiriki laana Zangu kuwa wasioweza kuokolewa na ni wale ambao wamemilikiwa na roho mbaya. Nina hamu ya kuwafukuza. Wamezaliwa na joka kuu jekundu na Ninawachukia zaidi. Kuanzia sasa kuendelea Siwahitaji wao kunitolea huduma zozote—Siwataki tu! Simtaki yeyote kati yao! Hata kulia kwao na kusaga meno mbele Yangu hakuna athari—nyinyi ni vitu gani? Je, unastahili kuja mbele Yangu? Je, unastahili? Bado wanajifanya kuwa watu wazuri na kujifanya kuwa wanyenyekevu! Baada ya kuyafanya mambo mengi mno mabaya, je, Ninaweza kukuhurumia? Na kuinuka mbele Yangu unaanza kuniasi tena. Hujawahi kuwa na nia yoyote nzuri na unataka tu kunilaghai Mimi! Je, unaweza kurejea na kuwa mzuri endapo wewe ni mzao wa joka kuu jekundu? Haiwezekani! Tayari umekwisha kulaaniwa na Mimi na Ninakuhukumu kabisa! Nifanyie huduma kwa moyo wako wote, kwa uaminifu na kwa njia iliyo na nidhamu, na kisha rudi kwenye shimo la kuzimu! Je, unataka sehemu katika ufalme Wangu? Unaota! Huna aibu! Wewe uliye na mwili wenye uchafu, takataka, uliyepotoshwa sana, ilhali bado una ujasiri wa kuja mbele Yangu! Ondoka! Ukichelewa hata kidogo Nitakuadhibu vikali! Wale wote wanaojihusisha na upotovu na udanganyifu mbele Yangu lazima wafunuliwe. Je, unaweza kujificha wapi? Je, mnaweza kujisetiri wapi? Je, mnaweza kuepuka udhibiti Wangu bila kujali utakwepa au kujificha kiasi gani? Usiponitolea huduma vema basi maisha yako yatakuwa mafupi hata zaidi—utamalizwa mara moja!
Ninawaambia dhahiri ni watu wa aina gani walio wazaliwa Wangu wa kwanza na Ninawapa mathibitisho sahihi. Nisingefanya hivyo, basi msingeweza kuchukua nafasi zenu zinazowafaa na mgejiamulia wenyewe pahali ambapo panawafaa. Wengine wangekuwa wanyenyekevu zaidi na wengine wangekuwa wenye kiburi zaidi, na wale wasiomiliki ubora Wangu, au wale ambao ubora wao unakosa kabisa wote wangetaka kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza. Je, ni maonyesho gani ambayo yanafanywa na wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza? Kwanza, wao husisitiza kuyaelewa mapenzi Yangu, wanadhukuru juu ya mapenzi Yangu na wakati huo huo wote wanashughulikiwa na Roho Mtakatifu; pili, wao huendelea kutafuta katika roho, wao si wenye kupotoka, wao huwa katika mipaka Yangu kila wakati, ni wa kawaida sana, na tabia hizo si za kuiga (kwa kuwa wanalenga kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na wanadhukuru juu ya upendo Wangu kwao, wao ni waangalifu katika kila wakati na wana hofu kuu ya kuwa na moyo ambao unanisaliti au kuniasi Mimi); tatu, wao hutenda kwa moyo wote kwa ajili Yangu, wana uwezo wa kutoa nafsi zao zote, na tayari wamekwisha kulifuta wazo lolote la matumaini yao ya baadaye, maisha yao, wanachokula, kuvaa, kutumia au wanapoishi; la nne, wao daima huwa na moyo ambao huwa na njaa na kiu ya haki, wao huamini kuwa wana upungufu mwingi na kuwa vimo vyao si pevu; la tano, ni wale ambao Nimewataja mbeleni, kuwa wale ambao wana sifa nzuri duniani lakini wametupwa kando na watu wa kidunia, na ambao wana uaminifu wa maadili katika mahusiano yao na jinsia tofauti. Haya yote ni uthibitisho, lakini sasa Siwezi kuwafunulia yote kabisa kwa kuwa kazi Yangu bado haijafikia hatua hiyo. Wazaliwa Wangu wa kwanza, kumbukeni! Hisia za maisha ndani yenu, uchaji wenu Kwangu, upendo wenu Kwangu, ufahamu wenu Kwangu, kutafuta kwa ajili Yangu, imani yenu—haya yote ni upendo Wangu kwenu na yote ni mathibitisho Ninayowapa, ili kwamba nyote kwa kweli muwe wana Wangu wapendwa na muwe kama Mimi, kula pamoja, kuishi pamoja, kufurahia baraka na Mimi katika utukufu usio na kifani!
Siwezi kumwonea huruma yeyote aliyenitesa, wale ambao hawakuwa na ufahamu juu Yangu (pamoja na kabla jina Langu kushuhudiwa), walioamini kuwa Mimi ni mwanadamu, vilevile wale walionikufuru na kunikashifu hapo zamani. Hata wakiwa na ushuhuda mkuu sana Kwangu sasa hivi, hilo halitasaidia. Kunitesa Mimi hapo mbeleni kulikuwa kunitolea huduma na bado wao ni ala Zangu kama watanitolea ushuhuda Wangu leo. Ni wale tu ambao kwa kweli wamefanywa wakamilifu na Mimi Mwenyewe wanaoweza kutumika nami, kwa kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye haki, na Nimetoka katika mwili na kujitenga na mahusiano yote ambayo ni ya dunia. Mimi ni Mungu Mwenyewe na watu wote, mambo yote, na vitu vyote vilivyokuwa vimenizunguka zamani vi mikononi Mwangu. Mimi sina hisia na Mimi hutenda uhaki kwa kila kitu. Mimi ni mwadilifu, Sijachafuliwa na hata chembe ya uchafu. Je, unayaelewa maana ya maneno Wangu? Je, unaweza kutimiza hili? Watu hufikiri kuwa pia Nina ubinadamu wa kawaida, familia na hisia, lakini, je, wajua kuwa umekosea kabisa? Mimi ni Mungu! Je, mmesahau hili? Je, mmechanganyikiwa? Bado hamnifahamu!
Haki Yangu imefunuliwa kwako kikamilifu. Njia yoyote ambayo Ninamshughulikia mtu wa aina yeyote yote hufunua haki Yangu na uadhama Wangu. Kwa kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye huja na ghadhabu, Sitaruhusu hata mmoja ambaye alinitesa au kunitukana aponee. Je, mnaona hili kwa udhahiri, chini ya matakwa haya makali? Wale ambao Mimi huwachagua na kuwajaalia ni kama lulu adimu ama ageti na ni wachache na waliotawanyika, kwa kuwa wale watakaotawala kama wafalme kwa hakika lazima wawe wachache zaidi kuwaliko wale ambao watakuwa watu Wangu, na hili linafichua nguvu Zangu na matendo Yangu ya ajabu. Mara nyingi Mimi husema kuwa Nitawatuza, kuwapa taji na ndani Yangu kuna utukufu usiokuwa na mwisho. Je, Ninamaanisha nini kwa kusema zawadi, taji na utukufu? Katika dhana za watu, zawadi ni vitu vya mwili, kama vile chakula, mavazi au vitu vinavyoweza kutumiwa, lakini huku ni kufikiria kwao kwa zamani; si kile Ninachomaanisha ila ni ufahamu wenye upuuzi. Zawadi ni vitu vinavyopatikana sasa hivi na ni sehemu ya neema. Lakini kuna baadhi ambavyo vinahusiana na raha za mwili, na wale wanaotoa huduma kwa ajili Yangu lakini hawajaokolewa pia wanaweza kujipatia furaha ya mwili (ingawa ni vitu vya mwili ambavyo bado vinatoa huduma Kwangu). Taji si beji ya ofisi. Hiyo ni kusema, si kitu cha mwili ambacho Ninawapa kwa ajili ya furaha yenu, lakini badala yake ni jina jipya ambalo Ninawapa, na wowote wanaoweza kulifikia jina lako jipya watakuwa wale ambao wamejipatia taji, ambayo ni kupata baraka Zangu. Zawadi na taji ni sehemu ya baraka, lakini zikilinganishwa na baraka, ni chache mno, kama vile tofauti kati ya mbingu na nchi. Utukufu hauwezi hasa kufikiriwa kwa dhana za watu, kwa kuwa utukufu sio vitu vya mwili, ila ni kitu ambacho wanawaza katika dhana zisizo na kadiri. Hivyo utukufu ni nini hasa? Ina maana gani kusema kuwa mtashuka kwa utukufu pamoja na Mimi? Uzima Wangu, yaani, kile Nilicho na kile Nilicho nacho—Huruma na upendo wenye wema (kwa wana Wangu), na haki, uadhama, hukumu, ghadhabu, kulaani na kuchoma (kwa watu wote)—nafsi Yangu ni uadhama. Kwa nini Ninasema kuwa Kwangu kuna utukufu bila mwisho? Ni kwa sababu Kwangu kuna hekima bila mwisho na utele usioweza kulinganishwa. Kwa hivyo, kupanda kwa utukufu na Mimi kunamaanisha kuwa tayari mmekwisha kufanywa mkamilifu na Mimi, mna kile Nilicho na kile Nilicho nacho, mnatimilizwa na Mimi, una moyo wa uchaji Kwangu na hamnipingi; mnapaswa kuelewa sasa, siyo?
Hali yenye wasiwasi ya mataifa yote ya kidunia imefika kileleni, na wote wanajitayarisha kwa kasi kutoa huduma kwa ajili Yangu na kupokea kuchoma Kwangu. Wakati ambapo ghadhabu Yangu na uchomaji vitawasili hakutakuwa na kidokezo kabla, ilhali Ninajua kile Ninachofanya na Niko dhahiri kabisa kukihusu. Mnapaswa kuwa na uhakika kuhusu maneno Yangu na lazima mfanye hima kutayarisha kila kitu, na kujitayarisha kuwachunga wale ambao huja kutafuta kutoka ughaibuni. Kumbuka hili! China—yaani, kila mtu na mahali ndani ya Uchina—vinapitia laana Yangu; je, mnaelewa maana ya maneno Yangu?
Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni