11/13/2017

Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo. Haijalishi ikiwa Anazungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, ama mwanadamu, ama mtu wa tatu—Mungu ni Mungu kila wakati na huwezi kusema kuwa yeye si Mungu kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu ambao Anazungumzia kutoka.  Kati ya baadhi ya watu dhana zimetokea kutokana na mitazamo tofauti tofauti ambayo Mungu Anazungumza. Watu hao hawana maarifa ya Mungu, na pia maarifa ya kazi Yake. Iwapo Mungu angezungumza kila wakati kutumia mtazamo mmoja, je mwanadamu hangeweka masharti kuhusu Mungu? Je Mungu Anaweza kukubali mwanadamu kutenda kwa njia hiyo? Haijalishi ni mtazamo gani ambao Mungu Anaongelea, Mungu Ana malengo Yake kwa kila moja. Iwapo Mungu Angeongea kila wakati kwa mtazamo wa Roho, ungeweza kushiriki na Yeye? Hiyvo, Anazungumza kupitia mtu wa tatu ili kukupatia maneno Yake na kukuongoza kwa ukweli. Kila kitu Atendacho Mungu kinafaa. Kwa ufupi, yote yanafanywa na Mungu, na hupaswi kuwa na shaka kuyahusu. Bora tu kwamba Yeye ni Mungu, basi haijalishi kuwa ni mtazamo gani Anaongelea kutoka, Yeye bado ni Mungu. Huu ni ukweli usiobadilika. Njia yoyote Afanyayo kazi, Yeye bado ni Mungu, na dutu Yake haiwezi kubadilika! Petro alimpenda Mungu sana na alikuwa mtu aliyetaka kumridhisha Mungu, lakini Mungu hakumshuhudia kama Bwana ama Kristo, kwani dutu ya kiumbe ni vile ilivyo, na haiwezi badilika. Katika kazi Yake, Mungu hafuati masharti, lakini Anatumia mbinu tofauti kufanya kazi Yake ifanikiwe na kuongeza maarifa ya mwanadamu kumhusu. Kila mbinu Yake ya kazi inamsaidia mwanadamu kumjua, na ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu kamili. Haijalishi ni mbinu gani ya kufanya kazi Yeye hutumia, kila ni ili kumwongeza mwanadamu na kumfanya mtimilifu. Ingawa moja ya mbinu Zake za kazi ilikaa kwa muda mrefu, ni kwa ajili ya kupunguza imani ya mwanadamu Kwake. Hivyo hampaswi kuwa na shaka. Hizi zote ni hatua za kazi ya Mungu, na mnapaswa kuzitii.

    Leo, kinachozungumziwa ni kuingia katika hali halisi. Hakuna mazungumzo ya kupaa mbinguni, ama kutawala kama wafalme; yote yazungumziwayo ni harakati za kuingia katika hali halisi. Hakuna njia ya utendaji ya kufuata kuliko hii, na kuongelea kutawala kama wafalme sio tendo la busara. Mwanadamu ana udadisi mkuu, na bado anapima kazi ya Mungu leo kupitia dhana zake za kidini. Baada ya kupitia mbinu nyingi za Mungu za kazi, mwanadamu bado hajui kazi ya Mungu, bado anatafuta ishara na maajabu, na bado anaangalia kama kazi ya Mungu imetimizwa. Je huu sio upofu mkuu? Bila kutimizwa kwa maneno ya Mungu, je bado ungeamini kuwa ni Mungu? Leo, watu wengi kama hao kanisani wanangoja kutazama ishara na maajabu. Wanasema, maneno ya Mungu yakitimizwa, basi yeye ni Mungu; maneno ya Mungu yasipotimizwa, basi yeye si Mungu. Je wewe basi unaamini Mungu kwa sababu ya kutimizwa kwa maneno Yake, ama kwa sababu ni Mungu Mwenyewe? Mtazamo wa mwanadamu wa kumwamini Mungu unafaa kurekebishwa! Unapoona kuwa maneno ya Mungu yametimizwa, unatoroka—je huku ni kuamini katika Mungu? Unapoamini katika Mungu lazima uache kila kitu kwa huruma za Mungu na utii kazi yote ya Mungu. Mungu Alizungumza maneno mengi sana katika Agano la Kale—ni yapi uliyoona kwa macho yako yakitimizwa? Unaweza kusema kuwa Yehova sio Mungu kwa sababu hujayaona hayo? Wakiona kwamba maneno ya Mungu hayajatimizwa, wengine hutaka kutoroka. Yule anayetaka kuondoka aondoke, hakuna anayewazuia! Jaribu, uone iwapo unaweza kutoroka. Baada ya kutoroka, bado tu utarudi. Mungu anakudhibiti na neno Lake, na ukiacha kanisa na neno la Mungu, hutakuwa na njia ya kuishi. Kama huamini haya, jaribu mwenyewe—unafikiri unaweza tu kuondoka? Roho wa Mungu Anakudhibiti, na huwezi kuondoka. Hii ni amri ya utawala wa Mungu! Kama kuna watu ambao wanataka kujaribu, basi, wanaweza! Unasema huyu mtu si Mungu, basi mtendee dhambi na uone Atakachofanya. Kuna uwezekano kuwa mwili wako hautakufa na bado utakuwa na uwezo wa kula na kuvaa mwenyewe, lakini mawazoni hutaweza kuvumilia; utakuwa na msongo na mateso, hakuna kitu kitakachokuwa uchungu zaidi ya hili. Mwanadamu hawezi kuvumilia kuadhibiwa mawazoni na kuvurugwa—labda unaweza kuvumilia kuumia kwa mwili, lakini huna uwezo wa kuvumilia dhiki ya mawazo na adhabu inayodumu kwa muda mrefu. Leo huwezi kuona ishara na maajabu yoyote, ilhali hakuna anayeweza kutoroka, kwani Mungu Anatumia neno Lake kumdhibiti mwanadamu. Yasiyoguzika, yasiyoonekana, bila majilio ya ukweli, ilhali mwanadamu bado hawezi kutoroka. Je haya si matendo ya Mungu? Leo, Mungu amekuja duniani kumpa mwanadamu maisha. Yeye hawezi kukubembeleza, vile watu wanavyofikiria kwa kukuonyesha ishara na maajabu ili kuhakikisha uhusiano wa amani kati ya Mungu na mwanadamu. Wale wote ambao lengo lao halielekei maisha, na badala yake wanakuwa makini kumfanya Mungu aonyeshe ishara na maajabu, ni Mafarisayo! Wakati huo, ni Mafarisayo ndio waliompiga Yesu misumari msalabani; ukimpima Mungu kulingana na mtazamo wa imani yako kwa Mungu, kumwamini Mungu maneno Yake yanapotimizwa, na kuwa na shaka na hata kumkufuru Mungu yasipotimizika, je basi huko si kumpiga misumari msalabani? Watu kama hao ni wazembe katika kazi zao, na wanasherekea kilafi kwa raha!

     Kwa upande mmoja, shida kubwa na mwanadamu ni kwamba haijui kazi ya Mungu. Ingawa tabia ya mwanadamu sio ile ya kukataa, ni ile ya shaka; hakatai, lakini pia hawezi kukiri kikamilifu. Watu wakiwa na maarifa kamilifu ya kazi ya Mungu, basi hawatatoroka. Kwa upande mwingine, ni kwamba mwanadamu hajui hali halisi. Leo, ni kwa neno la Mungu, ndio kila mmoja ameshiriki; hakika, baadaye usingoje kuona ishara na maajabu. Nawaambia wazi wazi: Katika hatua ya sasa, kile una uwezo wa kuona ni maneno ya Mungu, na ingawa hakuna jambo la hakika, maisha ya Mungu bado inaweza kuundwa ndani ya mwanadamu. Ni kazi hii ndiyo kazi kuu ya Ufalme wa Milenia, na iwapo huwezi kuiona kazi hii, basi utakuwa mnyonge na kuanguka chini, utateremeka kukiwa na majaribu na zaidi ya haya, utachukuliwa kama mfungwa na Shetani. Mungu Amekuja ulimwenguni hasa kuzungumza maneno Yake; unachoshiriki nacho ni neno la Mungu, uonacho ni neno la Mungu, usikiacho ni neno la Mungu, unachokaa nacho ni neno la Mungu, unachopitia ni neno la Mungu, na Mungu aliyepata mwili huyu kimsingi hutumia neno kumfanya mwanadamu kamili. Yeye haonyeshi ishara na maajabu, na hasa hafanyi kazi ambayo Yesu Alifanya hapo awali. Ingawa wao ni Mungu, na wote ni mwili, huduma Zao sio sawa. Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, kuleta ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, "Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba." Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvu, na kumfanya aweze kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa. Leo ni kazi gani ambayo Mungu katika mwili atakamilisha? Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya "Neno kuonekana katika mwili," kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe kuwa kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. Kuna wakati ambapo watu wengine humpinga Mungu. Mungu hasababishi ukosefu mkubwa wa starehe kwako, mwili wako hauadibiwi wala wewe kupitia ugumu—lakini pindi tu neno Lake linapokuja juu yako, na kukutakasa, hutaweza kuvumilia. Je si hivyo ndivyo ilivyo? Wakati wa "watendaji huduma" Mungu Alisema mwanadamu atupwe katika shimo lisilo na mwisho. Mwanadamu aliweza kufika kwenye shimo lisilo na mwisho? Kupitia kwa maneno tu kumtakasa mwanadamu, mwanadamu aliingia kwenye shimo lisilo na mwisho. Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. Kazi ya Mungu nyingi katika wakati huu wote imekuwa kutoa, ufunuo, na kushughulika. Hatoi laana kwa mwanadamu kijuu juu, na hata Akifanya hivyo, ni kupitia kwa neno. Na hivyo, katika enzi hii ya Mungu kuwa mwili, usijaribu kuona Mungu akiponya wagonjwa na kufukuza mapepo tena, usijaribu kila mara kuona ishara—hakuna haja! Ishara hizo haziwezi kumfanya mwanadamu kamili! Kuongea wazi: Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama ukweli huu wa kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia. Badala ya kulenga vitu vilivyo vibaya, mnapaswa tu kulenga yale yaliyo mazuri—hivyo ni kusema, bila kujali kama maneno ya Mungu yamekamilika au la, ama iwapo kuna majilio ya ukweli ama haupo, Mungu anamfanya mwanadamu kupata uzima kutoka kwa maneno Yake, na hii ndiyo ishara kuu kushinda zote, na hata zaidi, ni ukweli usiopingika. Huu ndio ushahidi bora wa kupata ufahamu kumhusu Mungu, na ni ishara hata kuu kushinda ishara. Maneno haya pekee yanaweza kumfanya mwanadamu kamili.

    Pindi tu Enzi ya Ufalme ilipoanza, Mungu alianza kuachilia Maneno Yote. Katika siku za baadaye, maneno haya yataendelea kutimizwa, na katika wakati huo, mwanadamu atakua katika uzima. Matumizi ya neno na Mungu kufichua tabia potovu ya mwanadamu ni ya kweli zaidi, na ni ya lazima zaidi, na Hatumii chochote ila neno kufanya kazi Yake ili kuifanya imani ya mwanadamu iwe kamili, kwani leo ni Enzi ya Neno, na inahitaji imani, uamuzi na ushirikiano wa mwanadamu. Kazi ya Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutumia neno Lake kutumikia na kukimu. Ni baada tu ya Mungu katika mwili kumaliza kuongea maneno Yake ndipo yatakapoanza kutimika. Wakati Anapoongea, maneno Yake hayatimiliki, kwani Anapokuwa katika hatua ya mwili, maneno Yake hayawezi kutimika, na hii ni ili mwanadamu aweze kuona kuwa Mungu ni mwili na sio Roho, ili mwanadamu aweze kutazama hali halisi ya Mungu kwa macho yake Mwenyewe. Katika ile siku ambayo kazi Yake imekamilika, wakati ambao maneno yote yanayopaswa kunenwa na Yeye duniani yamemenenwa, maneno Yake yataanza kutimika. Sasa sio enzi ya utimizaji, kwa kuwaHajamaliza kuongea maneno Yake. Kwa hivyo ukiona kuwa Mungu bado Ananena maneno yake duniani, usingoje utimizo wa maneno Yake; Mungu Anapokoma kunena maneno Yake, na wakati kazi Yake duniani imekamilika, huo ndio utakuwa wakati ambao maneno Yake yanaanza kutimika. Katika maneno Anayozungumza duniani, kunayo, katika mtazamo mmoja, utoaji wa uzima, na katika mtazamo mwingine, kuna unabii—unabii wa vitu vitakavyokuja, wa vitu vitakavyofanywa, na vya vitu ambavyo bado havijatimizwa. Kulikuwa pia na unabii katika maneno ya Yesu. Katika mtazamo mmoja, Alitoa uzima, na katika mtazamo mwingine Alinena unabii. Leo, hakuna mazungumzo ya kutekeleza maneno na uhakika kwa wakati mmoja, kwani tofauti kati ya yale yanayoweza kuonekana na macho ya mwanadamu na yale yanayotendwa na Mungu ni kubwa mno. Inaweza kusemwa tu kwamba, mara kazi ya Mungu inapokamilika, maneno Yake yatatimika, na mambo ya hakika yatakuja baada ya maneno. Duniani, Mungu katika mwili wa siku za mwisho anafanya huduma ya neno, na kwa kufanya huduma ya neno, Anazungumza maneno pekee, na hajali kuhusu mambo mengine. Mara kazi ya Mungu itakapobadilika, maneno Yake yataanza kutimika. Leo, maneno yanatumiwa kwanza kukufanya mkamilifu; Atakapopokea utukufu katika ulimwengu mzima, utakuwa wakati ambao kazi Yake imekamilika, wakati maneno yote ambayo yanapaswa kuzungumzwa yatakuwa yamezungumzwa, na maneno yote yamekuwa ukweli. Mungu amekuja duniani wakati wa siku za mwisho ili kutekeleza huduma ya neno ili mwanadamu amtambue, na ili mwanadamu aone kile Alicho, na aone hekima Yake na matendo Yake yote ya maajabu kutoka kwa neno Lake. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno kimsingi kushinda watu wote. Baadaye neno Lake litakuja katika kila dini, kikundi, taifa na madhehebu; Mungu hutumia neno kushinda, kuwafanya wanadamu wote waone kuwa neno Lake lina mamlaka na nguvu—na kwa hivyo leo, mnakumbana tu neno la Mungu.

     Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Bibilia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, "Neno kuonekana katika mwili"; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. "Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili." Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapunziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaifanyikia Misiri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.

      Nimesema hapo awali kuwa "Wale wote wanaotafuta kuona ishara na maajabu watatelekezwa; wao sio wale wataofanywa wakamilifu." Nimenena maneno mengi sana, ilhali hauna maarifa hata kidogo ya kazi hii, na kuwa umefika katika hatua hii, bado unaulizia ishara na maajabu. Je, kuamini kwako kwa Mungu ni harakati ya kuona ishara na maajabu, au ni kwa sababu ya kupata uzima? Yesu pia Alinena maneno mengi ambayo, leo, bado hayajatimika. Je unaweza kusema kuwa Yesu sio Mungu? Mungu alishuhudia kuwa Yeye ni Kristo na ni Mwana mpendwa wa Mungu. Je unaweza kukataa haya? Leo, Mungu anazungumza tu maneno, na iwapo huna uwezo wa kufahamu kabisa, basi huwezi kusimama kidete. Je unamwamini kwa sababu Yeye ni Mungu, au unamwamini kwa msingi kwamba maneno Yake yatatimika au la? Je unaamini katika ishara na maajabu, au unaamini katika Mungu? Leo, Haonyeshi ishara na maajabu—je Yeye kweli ni Mungu? Iwapo maneno Anayonena hayatimiki, je Yeye kweli ni Mungu? Je dutu ya Mungu inaamuliwa na iwapo maneno Anenayo yatatimika au hapana? Ni kwa nini watu wengine daima hungoja kutimika kwa maneno ya Mungu kabla ya kumwamini? Je hii si maana kwamba hawamjui? Wote walio na dhana za aina hii ni watu wanaomkana Mungu; wanatumia dhana kumpima Mungu; maneno ya Mungu yakitimika wanamwamini Mungu, na yasipotimika hawamwamini Mungu; na kila wakati wanatafuta ishara na maajabu. Je wao si Mafarisayo wa wakati wa sasa? Kama unaweza ama huwezi kusimama imara kunategemea iwapo unamjua ama humjui Mungu wa kweli—hili ni muhimu! Jinsi ulivyo ukuu wa uhalisi wa neno la Mungu ndani Yako, ndivyo ulivyo ukubwa wa maarifa yako kuhusu uhakika wa Mungu, na ndivyo utaweza kusimama kidete katika majaribu. Zaidi unavyotazamia ishara na maajabu, ndivyo utakavyokosa kusimama imara, na utaanguka katika majaribu. Ishara na maajabu sio msingi; uhakika wa Mungu tu ndio uzima. Watu wengine hawajui matokeo yanayotokana na kazi ya Mungu. Wanaishi katika mshangao kila siku, wakikosa kutafuta ufahamu wakazi ya Mungu. Harakati zao ni kumfanya Mungu atimize mapenzi yao, na ni baada tu ya haya ndio wawe makini katika imani yao. Wanasema kuwa watautafuta uzima iwapo maneno ya Mungu yatatimika, lakini iwapo maneno ya Mungu hayatatimika, basi hakuna uwezekano wa wao kuutafuta uzima. Mwanadamu anafikiri kuwa imani kwa Mungu ni kutafuta kuona ishara na maajabu na harakati ya kupanda mbinguni na mbingu ya tatu. Hakuna asemaye kuwa imani yake kwa Mungu ni harakati ya kuingia katika ukweli, kutafuta uzima, na kutafuta kupatwa na Mungu. Harakati ya aina hii ina thamani gani? Wale wasiofuata ufahamu waMungu na kuridhika kwa Mungu ni watu ambao hawamwamini Mungu, ni watu ambao hukufuru Mungu!

     Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi. Leo, aina hiyo ya utendaji wa kidini lazima itakaswe; kufuata udhihirisho wa miujiza ya Mungu, kufuata uponyaji wa Mungu na kukemea Kwake mapepo, kufuata kupewa amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu, kufuata kupata mandhari na raha ya mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini, sio dhahiri na ni njia dhahania ya imani. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: ni imani katika Mungu ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.

    Mungu anafanya kazi Yake katika ulimwengu mzima. Wote wanaoamini katika Yeye lazima walikubali neno Lake, na kula na kunywa neno Lake; hakuna atakayepatwa na Mungu kwa kuona ishara na maajabu yanayoonyeshwa na Mungu. Katika enzi zote, Mungu ametumia neno kila wakati kumfanya mwanadamu mkamilifu, hivyo hampaswi kuweka mawazo yenu yote kwa ishara na maajabu, ila unapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu alinena baadhi ya maneno, na katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena maneno mengi. Baada ya Yesu kumaliza kunena maneno haya mengi, mitume na manabii ambao walikuja baadaye walifanya watu watende kulingana na sheria na amri zilizowekwa na Yesu, na wakawafanya waishi kulingana na kanuni zilizonenwa na Yesu. Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu. Mwanadamu anapofanywa mkamilifu katika wakati ambao Mungu Anamaliza enzi katika siku za mwisho, atakuwa amehitimu kuona ishara na maajabu. Unapokuwa na maarifa ya Mungu na unaweza kumtii Mungu bila kujali Anachofanya, utaona ishara na maajabu, kwani hautakuwa na dhana kuhusu ukweli wa Mungu. Kwa sasa, wewe ni mpotovu na huwezi kuwa na utiifu kamili kwa Mungu—je umehitimu kuona ishara na maajabu? Wakati ambao Mungu anaonyesha ishara na maajabu ndio wakati ambao Mungu anamwadhibu mwanadamu, na pia wakati ambao enzi inabadilika, na zaidi, wakati ambao enzi inatamatika. Wakati ambao kazi ya Mungu inatekelezwa kama kawaida, Haonyeshi ishara na maajabu. Kuonyesha ishara na maajabu ni jambo rahisi mno, lakini hiyo si kanuni ya kazi ya Mungu, wala si lengo la usimamizi wa Mungu wa mwanadamu. Iwapo mwanadamu angeona ishara na maajabu, na kama mwili wa kiroho wa Mungu ungemtokea mwanadamu, je watu wote hawangeweza "kuamini" katika Mungu? Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa. Je maneno haya yana maana gani? Yanamaanisha kuwa watu hao ambao wamepatwa waliamini kwa kweli tu baada ya kupitia hukumu na kuadibu, na kushughulikiwa na kupogolewa, na aina yote ya usafishaji. Imani ya watu kama hao sio isiodhahiri na dhahania, bali ni ya kweli. Hawajaona ishara na maajabu yoyote, ama miujiza yoyote; hawazungumzi kuhusu barua ngumu kueleweka na kanuni, ama mitazamo ya muhimu sana; badala yake, wana ukweli, na maneno ya Mungu, na maarifa ya kweli kuhusu ukweli wa Mungu. Je kikundi hiki hakina uwezo wa kuweka wazi nguvu za Mungu? Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni ya uhakika. Katika enzi ya Yesu, hakuja kumfanya mwanadamu awe kamili, ila kumkomboa mwanadamu, na hivyo Alionyesha miujiza kadhaa ili kufanya watu wamfuate. Kwani Yeye hasa Alikuja kukamilisha kazi ya kusulubiwa, na kuonyesha ishara haikuwa sehemu ya huduma Yake. Ishara na maajabu hayo yalikuwa ni kazi ambayo yalifanyika ili kufanya kazi Yake iwe na matokeo ya kufaa; hayo yalikuwa tu kazi ya ziada, na hayakuwakilisha kazi ya enzi nzima. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu pia Alionyesha ishara na maajabu kadhaa—lakini kazi Anayofanya Mungu leo ni kazi halisi, na kwa uhakika hawezi kuonyesha ishara na maajabu sasa. Punde alipoonyesha tu onyesha ishara na maajabu, kazi Yake halisi ingetupwa nje ya mpangilio wake, na hataweza kufanya kazi nyingine zaidi. Iwapo Mungu angesema neno litumiwe kumfanya mwanadamu kuwa kamili, lakini pia Aonyeshe ishara na maajabu, basi mwanadamu kumwamini ama kutomwamini kweli kungeweza kuwekwa wazi? Hivyo, Mungu hafanyi vitu vya aina hiyo. Kuna udini mwingi sana katika mwanadamu; Mungu amekuja katika nyakati za mwisho ili kutoa dhana zote za kidini na vitu visivyo vya kidunia ndani ya mwanadamu, na kumfanya mwanadamu ajue ukweli wa Mungu. Amekuja kutoa picha ya Mungu ambayo ni ya dhahania na bunifu—picha ya Mungu ambaye, kwa maneno mengine, hayupo hata kidogo. Na hivyo, sasa kitu cha pekee kilicho cha thamani ni wewe kuwa na ufahamu kuhusu hali halisi! Ukweli unashinda kila kitu. Unamiliki ukweli kiasi gani leo? Je, kila kitu kinachoonyesha ishara na maajabu ni Mungu? Roho wabaya pia wanaweza kuonyesha ishara na maajabu; je, hawa wote ni Mungu? Katika imani yake kwa Mungu, kile anachotafuta mwanadamu ni ukweli, anachotafuta ni uzima, na sio ishara na maajabu. Hivi ndivyo linavyopaswa kuwa lengo la wote wanaoamini katika Mungu.

                                       kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

 Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa MasharikiAsili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni