1/11/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Nane

Mwenyezi Mungu alisema, Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambao watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu.

1/10/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

 Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Saba


Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:
Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmekuwa mkiyasikia maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mnayo matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, mapenzi yake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotawazawa na Mimi.

1/09/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Sita 

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. 

1/08/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Tano


Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu?

1/07/2018

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song



Utambulisho

Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu
Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote,
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
jua linaaangaza kotekote.

1/06/2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu


Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha.

1/05/2018

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki


Utambulisho


Nitampenda Mungu Milele
Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini Hujawahi kuniacha.