Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya
Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi?