10/14/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu 

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kazi ya Mungu, Umeme wa Mashariki

Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu

Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.

10/13/2018

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Roho Mtakatifu, Umeme wa Mashariki

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hiyo ni kusema, Agano la Kale, Agano Jipya, na Biblia ya Enzi ya Ufalme–Neno Laonekana Katika Mwili–zilizoonyeshwa Bwana Yesu aliyekurudi wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ni imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.

10/12/2018

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova.

10/11/2018

Mchezo Mfupi wa Kuchekesha | "Njama za Polisi" (Swahili Subtitles)



 Mchezo Mfupi wa Kuchekesha | "Njama za Polisi" (Swahili Subtitles)


Utambulisho
Ili kuondoa imani za dini, serikali ya CCP ambayo inakana Mungu mara kwa mara inatumia mikakati ya kuchunguza Wakristo kama vile kuendesha uchunguzi wa siri na kufuatilia ili kuwafutilia mbali wote. Kichekesho cha Njama za Polisi kinahusu ushirikiano wa maafisa waovu wa CCP katika sura fiche na ofisa msaidizi, punda anayevaa ngozi ya simba, anayeendesha ufuatiliaji wa siri wa kuwatia mbaroni Wakristo wanaokusanyika kwenye nyumba ya Zhao Yuzhi. Je, Zhao Yuzhi na familia yake watashughulikiaje njama ovu za polisi wa Kichina? Je, ni shida gani zitakazowakumba wao?
    Yaliyopendekezwa: Kuhusu Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

10/10/2018

Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ushuhuda, Umeme wa Mashariki


Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa

Yixin
Kijiji cha kishamba kilichojikokota kimaendeleo, wazazi wangu waliochoka kwa sababu ya kazi zao, maisha ya shida za kifedha … kumbukumbu hizi za huzuni zilitia alama kwa mawazo yangu machanga, zilikuwa ni hisia yangu ya kwanza ya “majaliwa.” Baada ya kuanza kwenda shule, mara ya kwanza nilipomsikia mwalimu wangu akisema kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” niliweka maneno haya imara mawazoni mwangu.

10/09/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ubia wa Kweli

66. Ubia wa Kweli

Fang Li    Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.

10/08/2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?



Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?


Utambulisho

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanasadiki kwamba maneno yote ya Mungu yako ndani ya Biblia, na chochote kilicho nje ya Biblia hakina kazi Yake na maneno. Hawatafuti nje ya Biblia matamko Yake katika kurudi Kwake. Je, wataweza kukaribisha kurudi kwa Bwana kama wataendelea kushikilia wazo hili? Je, Mungu angeweza kuzuiliwa tu kwa kuongea maneno yaliyo ndani ya Biblia?