NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA: SAA YA GIZA KABLA YA MAPAMBAZUKO (Ukuzaji) | KANISA LA MWENYEZI MUNGU
Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini.
Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inaelezea uzoefu wa kweli wa Mkristo Mchina, Yang Huizhia, ambaye alikamatwa na serikali CCP, akateswa, na kufa kutokana na kuteswa kwake kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Baada ya Yang Huizhi kufa, serikali ya CCP kwa uongo ilidai kuwa kifo chake kilikuwa kimetokana na mshtuko wa moyo. Familia yake ilitaka kutafuta haki kwa ajili yake, lakini hatimaye walishtuka hadi kutulia kwa sababu ya vitisho vya CCP.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni