1/17/2018

Tamko la Kumi na Tatu|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Tamko la Kumi na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Ijapokuwa nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna aliyefahamu? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu Nimejivisha ubinadamu wa mwanadamu wa kawaida na kujivika ngozi ya mwanadamu, wanadamu hulitambua umbo Langu tu kwa nje ila hawatambui uhai uliomo ndani Yangu, wala hawatambui Mungu Roho, wanajua tu mtu wa mwili. Je, yawezekana kuwa Mungu halisi Mwenyewe hana thamani kwako kujaribu kumfahamu? Yawezekana kuwa Mungu halisi Mwenyewe hana thamani kwako kujaribu “kumhakiki kwa makini”? Nachukizwa na upotovu wa ukoo mzima wanadamu, lakini nauonea imani unyoge wao. Vilevile Ninashughulikia tabia kongwe ya wanadamu. Kama mmoja wa watu Wangu katika Uchina, wewe si sehemu ya wanadamu? Miongoni mwa watu Wangu Wote, na miongoni mwa Wanangu wote, yaani, miongoni mwa wale Niliowachagua kutoka kwa wanadamu wote, unapatikana katika kundi la chini zaidi. Kwa sababu hii, Nimegharamika kwa nguvu nyingi zaidi kwako, na juhudi nyingi. Je, bado huyathamini maisha ya baraka uliyonayo sasa? Je, bado unafanya moyo wako kuwa mgumu na kuasi dhidi Yangu na kuenenda katika mipangilio yako mwenyewe? Isingekuwa kwamba bado Nina huruma na upendo kwenu, wanadamu wote wangekuwa wameshakuwa mateka wa Shetani na kugeuka kuwa “mafunda matamu” katika kinywa chake. Leo hii, miongoni mwa wanadamu wote, wale wanaogharimia kwa dhati kwa ajili Yanguna wale wanaonipenda kwa dhati ni adimu sana kiasi cha kuwahesabu kwa vidole vya mkono mmoja. Yawezekana kuwa jina[a]“watu Wangu” limekuwa miliki yako binafsi? Je, dhamiri yako imeingia ubaridi? Je, unafaa kweli kuwa mtu Ninayehitaji? Kwa kutafakari kuhusu zamani, halafu sasa, ni nani kati yenu ameufurahisha moyo Wangu? Ni nani kati yenu ameonyesha kutaka kujihusisha na dhamira Yangu kihalali? Kama Mimi Singewazindua, bado usingeamka, lakini, mngeendelea kuwa kama mlioganda, na tena, katika hali ya kubumbwaa.

Katikati ya mawimbi mabaya, mwanadamu huiona ghadhabu Yangu; katika dhoruba na mawingu meusi, wanadamu huogopeshwa kiasi cha kuwa na wazimu, wasijue pa kukimbilia, kana kwamba radi na mvua zitawasomba. Halafu, baada ya kupita kwa dhoruba ya theluji, hali zao zinakuwa tulivu na zenye furaha zikipendezwa na urembo wa mandhari ya asil. Lakini, katika hali hizo, ni nani kati yao amewahi kushuhudia mapenzi Yangu yasiyo na kikomo Niliyo nayo kwa mwanadamu? Katika mioyo yao ni umbo Langu tu, ila si kiini cha Roho Wangu: Yawezekana kwamba mwanadamu hanikatai hadharani? Tufani ikishapita wanadamu wote huwa kama walitengezwa upya, kana kwamba, walitakaswa kupitia kwa masaibu wakapata tena mwangaza na uhai. Je, hukuwa na bahati njema kuiona leo baada ya kupitia mapigo yote Niliyokupa? Lakini leo ikiisha na kesho kuwadia, utaweza kuendelea kudumisha utakatifu uliofuata mvua hiyo? Utaweza kuendelea kuwa na moyo wa ibada uliofuata usafishaji wako? Utaendelea kuwa na usikivu wa leo? Ibada yako yaweza kuendelea bila kukoma au kubadilika? Kwa hakika hili si sharti lililo nje ya uwezo wa mwanadamu. Ninaishi na wanadamu siku baada ya siku nikitenda pamoja nao, katikati ya wanadamu, ila hapana hata mmoja aliyegundua hili. Isipokuwa uongozi wa Roho Wangu, ni nani kati ya ukoo mzima wa wanadamu bado angekuwepoi katika enzi hii? Yawezekana Ninatia chuku Ninaposema kuwa naishi na kutenda miongoni mwa wanadamu? Zamani Nilisema kuwa “Niliwaumba binadamu, na kuwaongoza wanadamu wote, na kuuamuru ubinadamu mzima”; hili halikuwa kweli? Inawezekana kuwa uzoefu wako wa haya mambo ni finyu? Kauli ya “mtendaji-huduma” inafaa kukutosha kugharamia juhudi zako maishani ukieleza. Bila uzoefu halisi, mwanadamu hawezi kunifahamu, hawezi kunifahamu kupitia katika maneno Yangu. Ila leo Nimekuja miongoni mwenu: Je, si hili litakurahisishia kunifahamu Mimi? Yawezekana kwamba kupata mwili Kwangu vilevile si ukombozi kwako? Kama Nisingeshuka kuja kwa mwanadamu Mimi binafsi, wanadamu wote wangekuwa wameingiliwa na Shetani na kuwa mali yake, kwa sababu unachokiamini ni sura ya Shetani na hakihusiani na Mungu kwa njia yoyote. Si huu ni ukombozi Wangu?
Shetani anapokuja mbele Yangu, sitetemeki kwa kuuogopa ukali wake, wala kumuogopa kwa sababu ya ubaya wa sura yake; Ninampuuza tu. Shetani akinijaribu, Ninauona ujanja wake na kumfanya kutoweka kwa haya na aibu. Shetani akipigana Nami na kujaribu kunipokonya wateule Wangu, Naingia kikamilifu katika mwili Wangu; na katika mwili Wangu Ninawakimu na kuwaongoza watu Wangu ili wasianguke na kupotea, na Nawaongoza katika kila hatua ya safari. Na Shetani aking’atuka kwa kushindwa, Nitakuwa nimetukuka na watu Wangu watakuwa wamenitolea ushuhuda angavu na mkubwa. Kwa hivyo, Nitachukua ninavyotumia kama foili[b]katika mpango Wangu wa usimamizi na kuvitupilia mbali hatimaye katika shimo lenye kina kisichofikika. Huu ndio mpango Wangu, hii ndiyo Kazi Yangu. Katika maisha yako, ipo siku itakuja ambayo utakumbana na hali kama hii: Je, utakubali bila kusita kuwa mateka wa Shetani, au utanikimbilia Nikuokoe? Haya ndiyo majaliwa yako mwenyewe, na sharti uyakirie kwa makini.
Maisha katika ufalme ni maisha ya watu na Mungu Mwenyewe. Binadamu wote wako katika ulinzi Wangu na wote wako vitani dhidi ya joka kuu jekundu. Ili kushinda hili pambano la mwisho, ili kulimaliza kabisa hili joka kuu jekundu ni sharti watu wote wajitolee asili zao kabisa Kwangu katika ufalme Wangu. Nisemapo “ufalme” Ninamaanisha maisha ambayo mtu anaishi chini ya uangalizi wa uungu na kuongozwa moja kwa moja Nami na kufundishwa Nami moja kwa moja ili kwamba maisha ya mwanadamu, japo yupo duniani, yawe kama yu mbinguni, mfano wa maisha ya mbingu ya tatu. Japo niko katika mwili Wangu, sikumbani na upungufu wa kimwili. Ni mara ngapi Nimekuja miongoni mwa wanadamu kusikiliza maombi, na ni mara ngapi Nimefurahia sifa zao ninapotembea miongoni mwao? Japo wanadamu hawajaugundua uwepo Wangu, nitaendelea na kazi Yangu kwa njia hii. Katika makao Yangu, ambayo ni sehemu Nilipojificha, hata hivyo, katika haya makao Yangu, Nimewashinda maadui Wangu wote; katika makao Yangu, Nimepata uzoefu wa kuishi duniani; katika makao Yangu, Ninalichunguza kila neno na tendo la mwanadamu, na kuchungulia na kuongoza wanadamu wote. Wanadamu wangejihusisha na dhamira Yangu, hivyo kuuridhisha moyo Wangu na kunifurahisha, kwa hakika ningewabariki wanadamu wote. Hili silo Ninalolikusudia kwa wanadamu?
Mwanadamu akiwa kwenye usingizi mzito, ni kwa mapigo Yangu ya radi tu ndipo wanaweza kuzinduka kutoka ndotoni mwao. Na wafunguapo macho yao, wengi huumizwa machoni na mwanga huu baridi, hadi kwa kiwango kwamba wanapoteza mwelekeo, na kushindwa kutambua watokako na waelekeako. Watu wengi hufumwa na mwanga huu na matokeo yake huanguka kwenye rundo chini ya dhoruba, na miili yao kusombwa na mafuriko, bila kuacha nyuma dalili yoyote. Katika mwangaza, manusura hatimaye huweza kuuona uso Wangu kwa uwazi zaidi, na hapo ndipo hugundua kitu kuhusu umbo Langu la nje, kwa kiasi kwamba wao hawawezi kudhubutu kuniangalia usoni ana kwa ana, wakihofu pakubwa kuwa Nitailetea tena miili yao kuadibu Kwangu na laana. Ni watu wangapi hulia kwa kwikwi nyingi? Ni wangapi hukata tamaa? Ni wangapi husababisha mito na damu yao? Ni wangapi huwa miili inayoelea huku na kule? Ni wangapi, wanapopata sehemu yao katika mwangaza, huumia mioyo yao ghafla na kulia machozi kwa ajili ya miaka yao ya kukosa furaha? Ni wangapi katika mwangaza huu wa kuogofya hukiri uchafu wao na kuahidi kubadili wenyewe mienendo yao? Ni wangapi, kwa kuwa wamepofushwa wamepoteza hamu ya kuishi na hatimaye hawawezi kamwe kuuona huu mwangaza na kwa hivyo kukwama, wakisubiri mwisho wao? Na ni watu wangapi waanza safari ya maisha yao na, chini ya uongozi wa mwanga huu, kwa bashasha wakitumainia kesho? ... Leo hii ni nani miongoni mwa wanadamu hayumo katika hali sawa na hii? Ni nani hayumo katika mwangaza Wangu? Hata kama wewe ni mwenye nguvu, au hata kama wewe ni mnyonge, ni vipi waweza kuepuka ujio wa mwanga Wangu?
Machi 10, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni