4/16/2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili


Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini
2. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

Mwenyezi Mungu anasema, “ Miongoni mwa dini hizi zote, mwisho wanaouzungumzia na kuupigania ni sawa na kupata uzima wa milele katika Ubudha—tofauti ni kuwa unapatikana kwa njia tofauti. Wote ni wa aina moja. Kwa hili kundi la watu wa dini hizi ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini katika tabia zao, Mungu huwapa hatima nzuri, sehemu nzuri ya kwenda, na kuwatendea inavyofaa. Haya yote ni sawa, ila si jinsi ambavyo watu wanadhani, siyo? Sasa, baada ya kusikia yanayowatokea Wakristo, mnajihisi vipi? Je, mnawasikitikia? Mnawahurumia? (Kidogo.) Hakuna linaloweza kufanywa—watajilaumu wenyewe. Kwa nini Ninasema hivi? Kazi ya Mungu ni ya kweli, Mungu yu hai na kweli, na kazi Yake inawalenga wanadamu wote na kila mtu—basi mbona Wakristo wasikubali hili? Ni kwa nini wanampinga kwa nguvu na kumtesa Mungu? Wana bahati hata kuwa na mwisho kama huu, basi mbona mnawaonea huruma? Kwa wao kutendewa namna hii kunaonyesha uvumilivu mkubwa. Kulingana na kiasi ambacho wanampinga Mungu, wanapaswa kuangamizwa—bali Mungu hafanyi hili, anaushughulikia Ukristo sawa tu na dini ya kawaida. Sasa kuna haja ya kutoa maelezo ya kina kuhusu dini nyinginezo? Maadili ya dini zote hizi ni kuwa watu wapitie shida zaidi, wasifanye maovu, waseme mambo mazuri, watende mambo mema, wasiwaapize watu wengine, wasifanye mahitimisho ya ghafla juu ya wengine, wajitenge na ugomvi, wafanye vitu vizuri, kuwa watu wazuri—mafundisho ya kidini mengi ni ya aina hii. Na kwa hiyo, kama hawa watu wa imani—hawa watu wa dini na madhehebu mbalimbali—wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, basi hawatafanya makosa au dhambi nyingi wakati wangali duniani, na baada ya kupata mwili mara tatu hadi saba, basi kwa jumla watu hawa, watu ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, watabaki kushikilia wajibu katika ulimwengu wa kiroho. Na je, kuna watu wengi wa aina hii? (La, hakuna wengi.) Jibu lako linategemea nini? Si rahisi kutenda mazuri, au kufuata amri na sheria. Ubudha haumruhusu mtu kula nyama—unaweza kufanya hilo? Ungepaswa kuvaa kanzu za kijivu na kukariri maandiko ya Kibudha katika hekalu la wafuasi wa Budha siku nzima, ungeweza kufanya hivyo? Haingekuwa rahisi. Ukristo una Amri Kumi za Mungu, amri na sheria, je, ni rahisi kufuata? Si rahisi! Chukua mfano wa kutowaapia wengine: Watu hawawezi kufuata hii amri. Kwa kushindwa kujizuia wenyewe, wanaapa—na baada ya kuapa hawawezi kurudisha kiapo, basi wanafanya nini? Usiku wanakiri dhambi zao. Wakati mwingine baada ya kuwaapia wengine, bado kuna chuki mioyoni mwao, na hata wanazidi zaidi na kupanga ni lini watawadhuru. Kwa jumla, kwa wale wanaoishi katika hii imani iliyokufa, si rahisi kukosa kufanya dhambi au kutenda maovu. Na kwa hiyo, katika kila dini, ni watu wachache tu ndio wanaweza kupata uzima wa milele. Unadhani kwamba kwa sababu watu wengi sana wanafuata hizi dini, wengi wataweza kubaki kuchukua nafasi katika milki ya kiroho. Lakini si wengi hivyo, ni wachache tu ndio wanaweza kulifikia hili. Kwa jumla ni hayo tu kwa mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani. Kinachowapambanua ni kwamba wanaweza kupata uzima wa milele, ambayo ni tofauti yao na wasioamini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni