6/05/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 67

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 67

Wana Wangu wanaonekana wazi, na wanaonekana mbele ya watu wote. Nitawaadhibu vikali wale wanaothubutu kuwakataa wao kwa wazi; hiyo ni hakika. Leo, wale wote wanaoweza kusimama na kuchunga kanisa wote sasa wamepata cheo cha wana wazaliwa wa kwanza na sasa wako pamoja katika utukufu Na Mimi—yale yote yaliyo Yangu ni yenu pia. Ninawakabidhi wale wanaonitii Mimi kwa dhati neema tele, ili uweze kuwa wenye nguvu, zaidi ya nguvu ya wanadamu wengine. Mapenzi Yangu yako juu yenu kwa ukamilifu wana wazaliwa wa kwanza na Nawatakia tu mkomae haraka iwezekanavyo na mkamilishe yale ambayo Nimewapa. Jua hili! Yale ambayo Nimewapa ni mradi wa mwisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Ninatarajia tu muweze kunipa Mimi nafsi yako yote kwa moyo wako wote, akili yako yote na nguvu yako yote, na utumie rasilmali kwa ajili Yangu. Muda kweli haumngoji mtu yeyote, na hakuna yeyote, au suala, na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuzuia kazi Yangu. Jua hili! Kazi Yangu inaendelea taratibu bila kizuizi katika kila hatua.

Nyayo Zangu zinatembea kote katika miisho ya ulimwengu, macho Yangu daima yanachunguza kila mtu, na hata zaidi Natazama picha yote ya ulimwengu. Maneno Yangu ya utendaji yanafika katika kila pembe ya ulimwengu. Yeyote anayethubutu kutotoa huduma yake Kwangu, yeyote anayethubutu kutokuwa mwaminifu Kwangu, yeyote anayethubutu kulihukumu jina Langu, na yeyote anayethubutu kuwatukana na kuwapaka tope wana Wangu—wale wote ambao kwa kweli wanafanya vitu hivi lazima wapitie hukumu kali. Hukumu Yangu inaanguka kikamilifu. Hivi ni kusema, sasa ni enzi ya hukumu, na kwa uchunguzi wa makini utapata kuwa hukumu Yangu inaendelea kote katika ulimwengu wa dunia. Bila shaka, familia Yangu haijaachwa; wale ambao fikira zao, maneno, na vitendo havipatani na mapenzi Yangu watahukumiwa. Lazima uelewe, hukumu Yangu inajumuisha ulimwengu wote wa dunia, sio tu kikundi kimoja cha watu ama vitu—je, umegundua hili? Kama kwa muda umekuwa na wazo lililopotoka, basi mara moja utapata hukumu ndani yako.
Hukumu Yangu huja kwa maumbo na aina zote. Jua hili! Mimi ni Mungu wa kipekee na wa busara wa ulimwengu wa dunia mzima! Hakuna kitu kinachozidi nguvu Yangu. Hukumu Zangu zote zimefichuliwa kwenu: Kama una mawazo yoyote yasiyo sahihi basi Nitakupa ufunuo. Yaani, Nitakuonya. Kama hutasikia, basi Nitakuacha mara moja (hili halihusu kushuku jina Langu, lakini kwa tabia za nje—zile zinazohusu raha za kimwili). Kama mawazo yako ni ya kunikataa, unanilalamikia, unakubali tena na tena mawazo ya Shetani na hufuati hisia za maisha, basi roho yako itakuwa gizani na mwili wako utapitia uchungu. Lazima uwe karibu na Mimi, hutaweza kabisa kurejesha hali yako ya kawaida kwa siku moja au mbili tu, na maisha yako yataonekana kubaki nyuma zaidi. Wale ambao hotuba yao haifai Nitaadhibu midomo yenu na ndimi na kufanya ndimi zenu kupitia ushughulikaji. Wale ambao bila kupinga ni wapotovu kwa matendo Nitawaonya kwa roho zenu, na Nitaadhibu vikali wale ambao hawasikii. Wale ambao wananihukumu na kunikana kwa wazi, yaani wale ambao wanaonyesha kutotii kwa neno ama kwa tendo, Nitawaondoa kabisa na kuwaacha, Nitawafanya kuangamia na kupoteza baraka za juu; hao ni wale ambao wanaondolewa baada ya kuchaguliwa. Wale ambao ni wajinga, yaani wale ambao maono yao sio wazi, bado Nitawapa nuru na kuwaokoa. Lakini wale ambao wanaelewa ukweli lakini hawauweki katika vitendo watapewa adhabu kulingana na sheria ambazo zimetajwa hapo juu, iwe hawajui au la. Kwa wale watu ambao nia zao hazijakuwa sahihi tangu mwanzo, Nitawafanya wasiweze milele kupata ukweli na wataondolewa hatua kwa hatua, mmoja kwa mmoja—hakuna hata mmoja atakayebaki—lakini wale wanaobaki wanafanya hivyo kwa mpango Wangu (kwani Sifanyi vitu kwa haraka, lakini kwa mtindo wa utaratibu).
Hukumu Yangu imefichuliwa kabisa, imelengwa kwa watu tofauti, na wote lazima wachukue nafasi zao zinazostahili. Ikitegemea ni sheria gani iliyovunjwa, Nitawaadhibu na kuwahukumu kulingana na sheria hiyo. Na kwa wale ambao hawako katika jina hili na hawamkubali Kristo wa siku za Mwisho, kuna sheria moja tu: Nitachukua roho mara moja, roho na mwili wa yeyote anayenikataa na kuwatupa Kuzimu; wowote ambao hawanikatai Mimi, Nitangoja mkomae kabla ya kufanya hukumu ya pili. Maneno Yangu yanaeleza yote kwa uwazi kamili na hakuna kilichofichwa. Ninatarajia tu kuwa mtaweza kuyaweka akilini kila wakati!
Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 67
Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni