7/03/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89
Sio rahisi kuwa sawa na makusudi Yangu kwa kila kitu unachofanya; sio jambo la kujilazimisha kudanganya, lakini inategemea ikiwa Nilikujalia na akili Yangu kabla ya kuumbwa kwa dunia, ambalo lilikuwa jukumu Langu. Hiki sio kitu watu wanachoweza kufanya. Nitampenda ninayempenda, na yeyote Ninayesema ni mzaliwa wa kwanza hakika ni mzaliwa wa kwanza, hii ni sawa kabisa. Unaweza kutaka kudanganya, lakini huku kutakuwa bure tu! Unadhani Sikutambui? Je, kuwa na tabia nzuri mbele Yangu inatosha? Je, ni rahisi hivyo? La hasha. Lazima uwe na ahadi Yangu, majaliwa Yangu. Je, unafikiri sijui unachokifanya nyuma Yangu? Umepotoshwa! Rudi haraka kwenye ziwa la moto na moto wa jehanamu mara tu utumishi wako Kwangu utakapoisha! Nimechukizwa, Ninajazwa na chuki kwa kukuona. Wote wanaonitumikia ambao hawatumii raslimali zao kwa uaminifu kwa ajili Yangu, ni wapotovu na wasiozuiwa, na hawatambui makusudi Yangu, baada ya utumishi wako kuisha, ondoka mbele ya macho Yangu! La sivyo Nitakutupa nje! Watu hawa hawawezi kuishi kwenye nyumba Yangu (kwa jina, kanisa) kwa muda zaidi. Lazima waondoke hapa ili kuzuia kutia jina Langu aibu, kuharibu sifa Yangu. Watu hawa wote ni wa ukoo wa joka kuu jekundu, wametumwa na joka kuu jekundu kuvuruga usimamizi Wangu. Wamebobea katika udanganyifu kuvuruga kazi Yangu. Wanangu! Ni lazima muone hili! Msishirikiane na watu hawa. Unapowaona watu wa aina hii nenda mbali nao kwa haraka ili kuzuia kutiwa kwenye mtego na hao na kuleta madhara katika maisha yako! Ninawachukia zaidi watu ambao huongea ovyo ovyo, wanaotenda bila kufikiria, wanaokuwa na mzaha tu na kucheka, wanaojihusisha na mazungumzo yasiyofaa. Siwataki watu hawa, wote ni wa namna ya Shetani! Kuchokoza bila sababu kabisa, je, hao ni nini? Kuongea na kufanya upuuzi, je, bado hawaoni aibu? Kwa uhalisi, mtu wa aina hii anachukuliwa kuwa wa thamani ya chini zaidi, kwa muda mrefu Nimewatazama, kwa muda mrefu Nimewatelekeza. La sivyo, kwa nini wanaongea upuuzi mara kwa mara bila ya Mimi kuwaadhibu? Wao kweli ni wa ukoo wa joka kuu jekundu! Sasa Nimeanza kuvitoa vitu hivi kimoja baada ya kingine. Je, Naweza kuwatumia wazaliwa wa Shetani kama wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume, kama wana Wangu na watu Wangu? Basi Sitakuwa nimechanganyikiwa? Hakika Sitafanya hivyo. Je, mnaelewa hili wazi?

Kila kitu mnachokumbana nacho leo, kiwe kizuri au kibaya, vyote vimepangwa kwa mikono Yangu yenye hekima: vyote vimepangwa, vimedhibitiwa na Mimi. Hakika hiki sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kuwa tayari kukifanya. Watu wengine bado wanatokwa jasho kwenye viganja vyao, wakiwa na wasiwasi kunihusu; kweli hawafai kuwa na wasiwasi! Wanaisahau kazi yao kuu, kutoingia katika roho ilhali wanataka kukua katika maisha; wanatumaini bure! Hawana wasiwasi kabisa, lakini bado wanataka kuridhisha makusudi Yangu! Una wasiwasi kwa niaba Yangu, lakini Mimi sina wasiwasi. Je, una wasiwasi ya nini? Una uzembe katika kazi yako Kwangu, huku ukidanganya wazi wazi. Ninakwambia! Nitamwondoa mtu wa aina hii kutoka kwenye nyumba Yangu kwanzia sasa. Hafai kunitumikia katika nyumba Yangu. Namchukia mtu wa aina hii kwa sababu ananikufuru kwa matendo yake. Iliposemekana “kukufuru dhidi Yangu ni dhambi isiyosameheka,” hii ilikuwa inamuashiria nani? Je, mnaelewa hili? Mtu wa aina hii anaamini kwamba hiyo shida bado haijawa mbaya sana ingawa ameshatenda dhambi. Kweli mtu huyu aliyechanganyikiwa ni kipofu, mjinga, na roho yake imetiwa kizuizi! Nitakutupa nje! (kwa sababu hili ni jaribu la Shetani Kwangu, Ninalichukia kiasi hiki na jambo hili limetajwa mara kwa mara, kila wakati linanikasirisha. Siwezi kuizuia, hakuna anayeweza kuisimamisha. Isingekuwa ni suala la wakati bado haujafika, Ningekuwa nimeshughulikia kitambo.) (Hii ni kuhusu ukweli kwamba kwa wakati huu kuna watu wengi ambao bado hawaamini kwamba wageni watatafuta kuijaza Uchina; hata sasa bado hawaamini, kuifanya hasira Yangu kuvurugika na kuchemka.)
Ni mtu wa aina gani anayeupendeza moyo Wangu nyumabni Mwangu? Huku ni kusema, kabla ya uumbaji ni aina gani ya watu Niliowajalia waishi milele katika nyumba Yangu? Je, mnajua? Je, mumefikiria ni aina gani ya watu Ninaopenda na aina gani ya watu Ninaowachukia? Nyumba Yangu ni ya watu walio na mawazo sawa na Mimi, wanaoshiriki nyakati nzuri na ngumu pamoja nami, huku ni kusema, watu wanaoshiriki katika baraka na magumu. Hawa watu wote wanaweza kupenda Ninachopenda na kuchukia Ninachochukia. Wanaweza kukiacha kile Ninachochukia. Nikisema hawataweza kula, wako tayari kushinda njaa ili kuridhisha makusudi Yangu. Watu wa aina hii wako tayari kusalia waaminifu Kwangu na kutumia raslimali zao kwa ajili Yangu, wanaweza kufikiria kuhusu jitihada Zangu za bidii, daima wakinifanyia kazi kwa bidii. Kwa hivyo, aina hii ya watu, Ninawapa cheo cha wazaliwa wa kwanza wa kiume, Nikiwapa kilakitu Nilicho nacho: Nina uwezo wa kuongoza makanisa yote, hili Ninawapa; Nina hekima, hii pia Ninawapa; Ninaweza kuteseka kwa kutenda ukweli, na pia Nitawapa watu hawa nia, kuwafanya wawe na uwezo wa kuteseka kwa kila kitu kwa ajili Yangu; Nina tabia nzuri na hii pia Nitawapa, kuwafanya kuwa kama Mimi kabisa, kusiwe na tofauti hata kidogo kabisa ili kwamba watu wataniona ndani yao. Sasa, Nauweka uungu Wangu wote ndani ya watu hawa kuwawezesha kuishi kulingana na kipengele kimoja cha uungu Wangu kamili, kuwa ufunuo Wangu kamili; hili ndilo kusudi Langu. Usitafute kuwa kama Mimi kwa vitu vya nje (kula kama Mimi, kuvaa nguo sawa na kama Mimi), haya yote hayana maana, na mtajipoteza tu mkivitafuta vitu hivi. Hii ni kwa sababu wale wanaotafuta kuniiga kwa nje ni kikaragosi wa Shetani, na bidii hii ni mbinu ya Shetani, ni lengo la Shetani. Unatafuta kuwa sawa na Mimi lakini unastahili? Nitakukanyaga mpaka ufe! Kazi Yangu inaendelea daima, ikienea kwa kila taifa duniani. Zifuate hatua Zangu kwa haraka!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni