Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

5/12/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 47

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 47

Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho.

1/05/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8


Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.