Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kidini. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kidini. Onyesha machapisho yote

11/07/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu anasema, "Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu huja hapa ulimwenguni kimatendo ili kufanya kazi Yake na kuwasiliana na watu ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, ni bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa vitendo.