Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-ni-Kimbilio-la-Nafsi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-ni-Kimbilio-la-Nafsi. Onyesha machapisho yote

2/11/2018

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu

Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi. Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani.