Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda kwa Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda kwa Mungu. Onyesha machapisho yote

3/31/2019

Neno la Mungu | Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote , mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli kabisa! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vikasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi. Ee, Mwenyezi Mungu! Wewe ni kila kitu, Wewe umetimiza kila kitu, na kila kitu kinakamilika na Wewe, vyote vinang’aa, vyote vimekombolewa, vyote viko huru, vyote viko imara na vyenye nguvu! Hakuna chochote kilichofichwa wala kufungwa, na Wewe mafumbo yote yanafumbuliwa.