Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uzima. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uzima. Onyesha machapisho yote

4/14/2019

Neno la Mungu | Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani! Katika pembe za mbali za dunia, kama mvua inayonyesha ndani ya kila pembe na kila mwanya, hakuna doa hata moja linalobaki, na inavyoosha wote kutoka kichwa hadi kidole, hakuna kinachojificha kutoka kwake wala hakuna mtu yeyote awezeya kujikinga kutoka kwake.