Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutofautisha-watu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutofautisha-watu. Onyesha machapisho yote

2/02/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 17

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 17

Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe.