11/15/2017

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. 

11/14/2017

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

 Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. 

11/13/2017

Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo. Haijalishi ikiwa Anazungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, ama mwanadamu, ama mtu wa tatu—Mungu ni Mungu kila wakati na huwezi kusema kuwa yeye si Mungu kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu ambao Anazungumzia kutoka.

11/12/2017

Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno | Kanisa la Mwenyezi Mungu


Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno

 Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. 

11/11/2017

Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. 

11/10/2017

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

11/09/2017

Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake


Mwenyezi Mungu alisema:Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu, na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; wanamheshimu tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata wanamstahi Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli.