11/29/2017

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili


Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia.

11/28/2017

Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia.

11/27/2017

Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu


Mwenyezi Mungu alisema, Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli.

11/26/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,

Wewe U Mwaminifu kwa Nani?


Mwenyezi Mungu alisema, Kila siku unayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yako na majaliwa yako, kwa hivyo unapaswa kufurahia kila ulicho nacho na kila dakika inayopita. Unapaswa kutumia muda wako vizuri ili uweze kujinufaisha, ili usije kuishi maisha haya bure. Pengine unajihisi kukanganyikiwa unaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yako si vile tu ulivyo sasa.

11/25/2017

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu



 Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki kamwe mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.

11/24/2017

Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako


Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia.

11/23/2017

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini



Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha.