2/12/2018

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu



Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu


Watu wa Mungu wanainuliwa mbele ya kiti Chake cha Enzi,
maombi mengi mioyoni mwao.
Mungu huwabariki wote wanaorejea Kwake;
wote wanaishi katika mwanga.
Omba Roho Mtakatifu alipe nuru neno la Mungu
ili kwamba tujue kikamilifu mapenzi ya Mungu.
Tunaomba watu wote walitunze sana neno la Mungu
na waje kutafuta kumjua Mungu.
Tunaomba Mungu atupe zaidi ya neema Yake,
ili tabia zetu ziweze kubadilika.

2/11/2018

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi. Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani.

2/10/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote.

2/09/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.

2/08/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote.

2/07/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asili yake na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani.

2/06/2018

Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki)


Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki)


Wimbo wa Kifuasi cha Dhati

Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.
Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.
Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote.
Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.
Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.
Hekima Yake, uadilifu Wake, nayapenda yote.
Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.
Moyo wake, Upendo wake, vimefanya nishindwe.