2/15/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. 

2/14/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Moja

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa marejesho Yangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulukane waliko na gharika hii ya urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini mwandadamu hajawahi kunitabua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utarijiri uliofichika ndani Mwangu.

2/13/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (1)

 Mbeleni, kulikuwa na kupotoka kwingi katika jinsi watu walipata uzoefu, na kungeweza hata kuwa kwa ajabu. Kwa sababu tu hawakuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, kulikuwa na maeneo mengi ambayo uzoefu wa watu ulienda kombo. Sharti la Mungu kwa mtu ni kwao kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Njia za mtu wa kisasa kuhusiana na chakula na mavazi, kwa mfano. Wanaweza kuvaa suti na tai na wanaweza kujifunza kiasi kuhusu sanaa ya kisasa, na katika muda wao wa ziada wanaweza kuwa na kiasi fulani cha fasihi na maisha ya burudani.

2/12/2018

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu



Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu


Watu wa Mungu wanainuliwa mbele ya kiti Chake cha Enzi,
maombi mengi mioyoni mwao.
Mungu huwabariki wote wanaorejea Kwake;
wote wanaishi katika mwanga.
Omba Roho Mtakatifu alipe nuru neno la Mungu
ili kwamba tujue kikamilifu mapenzi ya Mungu.
Tunaomba watu wote walitunze sana neno la Mungu
na waje kutafuta kumjua Mungu.
Tunaomba Mungu atupe zaidi ya neema Yake,
ili tabia zetu ziweze kubadilika.

2/11/2018

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi. Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani.

2/10/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote.

2/09/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.