Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Sita
Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?” wakati ambapo fikira hii, wazo hili huumbika ndani ya akili zao, wao hung’ang’ana kulishinda kwa nguvu zao zote.