3/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I - Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I - Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu


3. Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu.
(Mwa 9:11-13) Na Nitalithibitisha agano langu nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika kuiharibu nchi. Na Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano Ninalofanya kati yangu na nyinyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote mpaka milele: Mimi Nauweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.
Watu wengi zaidi wanajua upinde wa mvua ni nini na wamesikia baadhi ya hadithi zinazohusiana na pinde za mvua. Kuhusiana na hadithi ile ya upinde wa mvua kwenye biblia, baadhi wa watu wanaisadiki, baadhi wanaichukulia tu kama hadithi ya kale, huku wengine hawaisadiki kamwe. Haijalishi ni nini, kila kitu kilichofanyika kuhusiana na upinde wa mvua ndicho kila kitu ambacho Mungu Alifanya hapo awali, na mambo yaliyofanyika katika mchakato huu wa usimamizi wa Mungu wa binadamu. Mambo haya yamerekodiwa vivyo hivyo kwenye Biblia. Rekodi hizi hazituambii chochote kuhusu hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo au nia zake nyuma ya maneno haya ambayo Mungu alisema. Zaidi, hakuna anayeweza kutambua ni nini Mungu alikuwa akihisi Aliposema maneno hayo. Hata hivyo, hali ya akili ya Mungu kuhusiana na hiki kitu chote inafichuliwa katikati ya mistari ya maandishi. Ni kana kwamba fikira zake wakati huo zinatoka kwenye ukurasa kupitia kila neno na kauli ya neno la Mungu.
Fikira za Mungu ni kile ambacho watu wanafaa kujali kuhusu na kile wanafaa kujaribu kujua zaidi. Hii ni kwa sababu fikira za Mungu zinahusiana kwa karibu na uelewa wa binadamu wa Mungu na uelewa wa binadamu wa Mungu ni kiungo muhimu sana kwa kuingia kwa binadamu katika maisha. Hivyo ni nini alichokuwa akifikiria Mungu wakati huo wakati mambo haya yalipofanyika?
Hapo mwanzo, Mungu aliuumba ubinadamu ambao katika macho Yake ulikuwa mzuri sana na karibu na Yeye, lakini waliangamizwa na gharika baada ya kuasi dhidi Yake. Je, ilimwumiza Mungu kwamba ubinadamu kama huo ulitoweke tu papo hapo hivyo? Bila shaka Aliumizwa! Kwa hivyo Maonyesho Yake ya maumivu haya yalikuwa nini? Ilirekodiwa vipi kwenye Biblia? Ilirekodiwa kwenye Biblia kama: “Na Nitalithibitisha agano langu nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika kuiharibu nchi.” Sentensi hii rahisi inafichua fikira za Mungu. Kuangamizwa huku kwa ulimwengu kulimpa Yeye maumivu sana. Kwa maneno ya binadamu, Alikuwa na huzuni sana. Tunaweza kufikiria: Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa maisha inavyofanana baada ya kuangamizwa na gharika? Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa binadamu inavyofanana hivi sasa? Hakuna makazi ya binadamu, hakuna viumbe walio hai, maji kila mahali na machafuko kabisa juu ya maji. Hilo ndilo lililokuwa onyesho la kusudio la asili Mungu wakati alipoumba ulimwengu? Bila shaka la! Nia asilia ya Mungu ilikuwa ni kuyaona maisha katika maeneo yote, kuwaona wanadamu Aliowaumba wakimwabudu Yeye, Si tu kwa Nuha kuwa mtu pekee anayemwabudu, au kuwa wa pekee ambaye angejibu mwito Wake ili kukamilisha kile alichoaminiwa kufanya. Wakati ubinadamu ulitoweka, Mungu hakuona kile alichonuia awali lakini kinyume cha mambo. Ni vipi ambavyo moyo Wake usingekuwa katika maumivu? Hivyo Alipokuwa akifichua tabia Yake na kuelezea hisia Zake, Mungu alifanya uamuzi. Ni aina gani ya uamuzi Alifanya? Kuunda uta mawinguni (kumbuka: upinde wa mvua tunaouona) kama agano na binadamu, ahadi kwamba Mungu hangemwangamiza mwanadamu na gharika tena. Wakati huohuo, ulikuwa pia ni kuwaambia watu kwamba Mungu aliwahi kuangamiza ulimwengu kwa gharika, kumfanya mwanadamu kukumbuka milele ni kwa nini Mungu alifanya kitu kama hicho.
Je, kuangamizwa kwa ulimwengu wakati huu kulikuwa ni jambo alilotaka Mungu? Bila shaka lilikuwa ni jambo asilotaka Mungu Huenda tukaweza kufikiria sehemu ndogo ya picha ile ya kusikitikia ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu lakini hatuwezi kukaribia kufikiria namna hali ilivyokuwa wakati huo mbele ya macho ya Mungu. Tunaweza kusema kwamba, haijalishi kama ni watu wa sasa au wa wakati huo, hakuna yeyote anayeweza kufikiria au kutambua ni vipi Mungu alikuwa akihisi Aliposhuhudia tukio hilo, picha hiyo ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwake na gharika. Mungu alilazimishwa kufanya haya kutokana na kutotii kwa binadamu, lakini maumivu ambayo moyo wa Mungu ulipitia kutokana na maangamizo haya ya ulimwengu kwa gharika ni uhalisia ambao hakuna anyeweza kuufikiria au kuutambua. Ndiyo maana Mungu aliweka agano na mwanadamu, ambalo lilikuwa ni kuambia watu kukumbuka kwamba Mungu aliwahi kufanya kitu kama hiki, na kuapa kwamba Mungu asingewahi kuangamiza ulimwengu kwa njia hii tena. Katika agano hili, tunauona moyo wa Mungu—tunaona kwamba moyo wa Mungu ulikuwa katika maumivu Alipouangamiza ubinadamu huu. Katika lugha ya binadamu, wakati Mungu aliangamiza mwanadamu na Akaona mwanadamu akitoweka, moyo Wake ulikuwa ukiomboleza na kuvuja damu. Je, hivyo sivyo tunavyoweza kuifafanua kwa njia bora zaidi? Maneno haya yanatumika na binadamu kuonyesha hisia za binadamu, lakini kwa sababu lugha ya binadamu inao ukosefu mwingi, kuitumia kufafanua hisia za Mungu hakuonekani kuwa mbaya sana kwangu Mimi, na wala si kubwa mno. Angaa inawapa uelewa sahihi kabisa, wa kufaa zaidi, wa hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo. Sasa mtafikiria nini mtakapouona upinde wa mvua tena? Angaa mtakumbuka namna ambavyo Mungu aliwahi kuwa katika huzuni kwa sababu ya kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Mtakumbuka namna, hata kama Mungu aliuchukia ulimwengu huu na kudhalilisha ubinadamu huu, Alipowaangamiza wanadamu Alioumba kwa mikono Yake mwenyewe, moyo Wake ulikuwa ukisononeka, ukipambana kuachilia, ukihisi kusita, na kuhisi vigumu kuvumilia mambo . Tulizo lake pekee lilikuwa katika familia ya wanane ya Nuhu. Ulikuwa ni ushirikiano wa Nuhu uliofanya jitihada Zake za kipekee za kuumba viumbe wote kuwa cha thamani. Kwa wakati ambao Mungu alikuwa akiteseka, hili ndilo jambo tu ambalo lingeweza kusawazisha maumivu Yake. Kuanzia hapo, Mungu aliweka matarajio Yake yote ya ubinadamu kwa familia ya Nuhu, akitumai kwamba wangeishi chini ya baraka Zake na si laana Yake, akitumai kwamba wasingewahi kumwona Mungu akiuangamiza ulimwengu kwa gharika na pia akitumai kwamba wasingeangamizwa.
Ni sehemu gani ya tabia ya Mungu tunayofaa kuelewa kutoka hapa? Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa ubinadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati ubinadamu ulikuwa umejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake , na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza ubinadamu huu. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hawakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya ubinadamu. Tunaona nini kutoka kwa haya? Bila shaka, tunaona kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kweli na si tu jambo ambalo Analizungumzia tu bila matendo. Ni jambo hakika, linaloweza kushikika na kutambulika, si bandia, halijatiwa najisi, halidanganyi wala halisingizii. Mungu kamwe hatumii uongo au kuunda taswira za bandia ili kufanya watu kuona kwamba Yeye anapendeka. Kamwe hatumii ushuhuda wa uongo ili kuwafanya kuona uzuri Wake, au kuringia uzuri wake na utakatifu Wake. Je, dhana hizi za tabia ya Mungu zinastahili upendo wa binadamu? Kwani nazo hazistahili kuabudiwa? Kwani nazo hazistahili kupendwa sana? Kwa sasa, Ningependa kuwaliza: Baada ya kuyasikia maneno haya, mnafikiri kwamba ukubwa wa Mungu ni tu maneno kwenye kipande cha karatasi? Je, uzuri wake Mungu ni maneno matupu tu? La! Bila shaka la! Mamlaka ya juu, ukubwa, utakatifu, uvumilivu, upendo, wa Mungu na kadhalika—dhana hizi zote mbalimbali za tabia ya Mungu na kiini chake zinaanza kutekelezwa kila wakati Anapoanza kazi Yake, zikiwa katika mapenzi Yake kwa binadamu, na pia zikitimizwa na kuonyeshwa kwa kila mtu. Licha ya kama umewahi kuzihisi awali, Mungu anamtunza kila mtu katika kila njia inayowezekana, kwa kutumia moyo Wake wa dhati, hekima, na mbinu mbalimbali ili kupashana mioyo ya kila mtu, na kuzindua roho ya kila mmoja. Huu ni ukweli usiopingika. Haijalishi ni watu wangapi wameketi hapa, kila mtu amekuwa na uzoefu tofauti na hisia tofauti kwa ustahimilivu, uvumilivu, na uzuri wake Mungu. Uzoefu huu wote wa Mungu na hisia hizi au utambuzi wa Yeye—kwa ufupi, mambo haya yote mazuri yanatoka kwa Mungu. Hivyo kwa kutangamanisha uzoefu wa kila mmoja na maarifa ya Mungu na kuziweka kwa pamoja na masomo yetu ya vifungu hivi vya Biblia leo, je sasa unao uelewa wa kialisia na bora zaidi kumhusu Mungu?
Baada ya kuisoma hadithi hii na kuelewa baadhi ya tabia za Mungu zilizofichuliwa kupitia kwa hafla hii, ni aina gani mpya kabisa ya shukrani mliyo nayo kwa Mungu? Je, imewapa uelewa wa kina zaidi wa Mungu na moyo Wake? Mnahisi tofauti sasa mnapoiangalia hadithi ya Nuhu tena? Kulingana na maoni yenu, ingehitajika kufanya mawasiliano ya mistari hii ya Biblia? Kwa vile tumewasiliana kuihusu, mnafikiria kwamba ilihitajika? Ilihitajika,sio? Ingawaje kile tulichosoma ni hadithi, ni rekodi ya kweli ya kazi ya Mungu ambayo aliwahi kuifanya. Nia yangu haikuwa kuwawezesha kufahamu maelezo ya hadithi hizi au mhusika huyu, wala haikuwa kwamba mweze kuenda kusomea kuhusu mhusika huyu, na bila shaka si eti mweze kurudi katika uchambuzi wa Biblia tena. Mnaelewa? Hivyo, hadithi hizi zimesaidia maarifa yenu ya Mungu? Hadithi hii imeongezea nini uelewa wenu wa Mungu? Twambie, kina kaka na kina dada kutoka makanisa ya Hong Kong. (Tuliona kwamba upendo wa Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kati yetu binadamu potovu anamilik.) Twambie, akina kaka na akina dada kutoka makanisa ya Korea. (Upendo wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli. Upendo wa Mungu kwa binadamu unao tabia Yake na unabeba ukuu Wake, utakatifu, uongozi, na ustahimilivu Wake. Kupitia hadithi kama hii tunaweza kushukuru kwa njia bora zaidi kwamba vitu vyote hivi ni sehemu ya tabia ya Mungu, na kwamba inafaa sisi tujaribu kupata uelewa wa kina zaidi.) (Kupitia kwa mawasiliano ambayo tumetoka kuwa nayo, kwa upande mmoja Ninaweza kuona haki ya Mungu na tabia ya kitakatifu, na Ninaweza pia kuona wasiwasi alionao Mungu kwa mwanadamu, rehema za Mungu kwa mwanadamu, na kwamba kila kitu anachofanya Mungu na kila fikira na wazo Alilonalo linafichua upendo na kujali Kwake kwa Ubinadamu.) (Uelewa wangu katika siku zilizopita ulikuwa kwamba Mungu alitumia gharika kuangamiza ulimwengu kwa sababu mwanadamu alikuwa amegeuka na kuwa mwovu kwa kiwango fulani, na ilikuwa ni kana kwamba Mungu aliuangamiza ubinadamu huu kwa sababu Aliuchukia. Ilikuwa tu baada ya Mungu kuzungumzia kuhusu hadithi ya Nuhu leo na Akasema ya kwamba moyo wa Mungu ulikuwa unavuja ndipo Ninatambua kwamba Mungu alikuwa kwa hakika shingo upande kuachilia ubinadamu huu. Ilikuwa tu ni kwa sababu mwanadamu alikuwa mtovu wa kusikia sana kiasi cha kwamba Mungu alikuwa hana chaguo lakini kumwangamiza. Kwa hakika, moyo wa Mungu wakati huo ulikuwa umesikitika sana. Kutoka haya Ninaweza kuona katika tabia ya Mungu utunzaji na kujali Kwake kwa mwanadamu. Hili ni jambo ambalo Sikujua awali. Nilikuwa nikifikiri ilikuwa ni kwa sababu mwanadamu alikuwa mwovu sana, na hivyo Mungu akawangamiza. Hivyo ndivyo uelewa wangu ulivyokuwa wa juujuu.) Vizuri sana! Mnaweza kwenda kwa kifuatacho. (Niliadhiriwa sana baada ya kusikiliza. Nimeisoma Biblia kitambo, lakini sijawahi kuwa na uzoefu kama leo pale ambapo Mungu anachambua kwa njia ya moja kwa moja mambo haya ili tuweze kumjua Yeye. Kwa Mungu kutushika mkono kuweza kuona Biblia inanifanya nijue kwamba kiini cha Mungu kabla ya kupotoshwa kwa binadamu kilikuwa ni upendo na utunzaji kwa mwanadamu. Tangu wakati ule binadamu alipopotoka hadi katika siku za mwisho za sasa, ingawaje Mungu anayo tabia ya haki, upendo na utunzaji Wake unabakia vilevile, haubadiliki. Hii inaonyesha kwamba kiini cha upendo wa Mungu, kuanzia uumbaji hadi sasa, licha ya kama binadamu amepotoka, haubadiliki. ) (Leo niliona kwamba kiini cha Mungu hakitabadilika kutokana na mabadiliko ya muda au mahali pa kazi Yake. Niliona pia kwamba, haijalishi kama Mungu anauumba ulimwengu au anauangamiza baada ya binadamu kupotoka, kila kitu Anachofanya kina maana na kinayo tabia Yake. Hivyo basi niliona kwamba upendo wa Mungu hauna kikomo na haupimiki, niliona pia, kama vile ambavyo wale kaka na dada wengine, utunzaji na rehema ya Mungu kwa mwanadamu wakati Alipouangamiza ulimwengu.) (Haya ni mambo kwa hakika sikuyajua kuhusu hapo awali. Baada ya kusikiliza leo, nahisi kwamba Mungu ni wa ajabu kwa kweli, wa kuaminika kwa kweli, anayestahili kusadikiwa, na kwamba kwa kweli Yupo. Ninaweza kutambua kwa dhati ndani ya moyo wangu kwamba tabia ya Mungu na upendo wa Mungu kwa kweli ni vitu vinavyoshikika. Hii ndiyo hisia niliyo nayo baada ya kusikiliza leo.) Safi kabisa! Yaonekana nyote mmechukua kile mlichosikia na kukitia moyoni.
Je, mmetambua ukweli fulani kutoka mistari yote ya Biblia, zikiwemo hadithi zote za Biblia tulizowasiliana leo? Je, Mungu amewahi kukutumia lugha Yake mwenyewe ili kuelezea fikira Zake binafsi au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa ubinadamu? Kunayo rekodi ya Yeye kutumia lugha ya kawaida kutaja ni kiasi kipi ambacho Anajali na Anapenda mwanadamu? La! Je, si hayo ni kweli? Kunao wengi sana miongoni mwenu ambao wamesoma Biblia au vitabu vingine bali na Biblia. Je, yupo yeyote kati yenu aliyeyaona maneno kama hayo? Jibu bila shaka ni la! Yaani, kwenye rekodi za Biblia, yakiwemo maneno ya Mungu au urekodi wa kazi Yake, Mungu hajawahi katika enzi yoyote au kipindi chochote kile kutumia mbinu Zake mwenyewe kufafanua hisia Zake au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa mwanadamu wala Mungu hajawahi kutumia matamshi au vitendo kufikisha hisia na mawazo Yake—Je, si hiyo ni ukweli? Kwa nini Ninasema hivyo? Kwa nini lazima Nitaje hii? Ni kwa sababu hii pia inayo uzuri wa Mungu na tabia Yake.
Mungu alimuumba mwanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi sana Wakena wala si makaragosi Yake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi. Wala Hahisi kwamba kuokoa ubinadamu, kuwatosheleza, na kuwapatia kila kitu, ni kutoa mchango mkuu kwa binadamu. Anamkimu tu mwanadamu kimyakimya na kwa unyamavu, kwa njia Yake mwenyewe na kupitia kwa kiini Chake na kile Anacho na alicho. Haijalishi ni toleo kiasi kipi na ni msaada kiasi kipi ambao wanadamu wanapokea kutoka kwa Yeye, Mungu siku zote hajawahi kufikiri kuhusu au kujaribu kutaka sifa yoyote. Hii inaamuliwa na kiini cha Mungu, na pia hasa ni maonyesho ya kweli pia ya tabia ya Mungu. Na ndio maana, haijalishi kama iko kwa Biblia au kitabu chochote kingine, hatujawahi kumpata Mungu akionyesha fikira Zake, na hatujawahi kumpata Mungu akifafanua au akitangazia wanadamu ni kwa nini Anafanya mambo haya, au ni kwa nini Anamjali sana mwanadamu, ili kumfanya mwanadamu kumshukuru Yeye au kumsifu Yeye. Hata wakati Amejeruhiwa, wakati moyo Wake umo katika maumivu makali, Hajawahi kusahau jukumu Lake kwa mwanadamu au wasiwasi Wake kwa mwanadamu, huku haya yote yakiendelea, Anavumilia madhara na maumivu akiwa pekee katika ukimya. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu anaendelea kumkimu mwanadamu kama Anavyofanya siku zote. Ingawaje mwanadamu mara nyingi humsifia Mungu au huwa na ushuhuda Kwake, hakuna kati ya tabia hii ambayo imedaiwa na Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kunuia mambo yoyote mazuri Anayomfanyia binadamu yeye pia naye kumfanyia vivyo hivyo kama ishara ya shukrani au ili iweze kuonekana kwamba anafanyiwa mazuri aliyofanya. Kwa mkono mwingine, wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu, wale wanaomfuata Mungu kwa kweli, wanaomsikiliza Yeye, na waliowaaminifu Kwake yeye, na wale wanaomtii Yeye—hawa ndio watu ambao mara nyingi watapokea baraka za Mungu, na Mungu atawakabidhi baraka hizo bila kusita. Isitoshe, baraka ambazo watu hupokea kutoka kwa Mungu mara nyingi zinazidi kufikiria kwao na pia zinazidi kitu chochote ambacho binadamu wanaweza kubadilishana na yale waliyofanya au gharama waliyolipia. Wakati mwanadamu anafurahia baraka za Mungu, Je, yupo yeyote anayejali ni nini Mungu anafanya? Je, yupo yeyote anayeonyesha wasiwasi wowote kuhusu vile ambavyo Mungu anahisi? Je, yupo yeyote anayethamini maumivu ya Mungu? Jibu la uhakika wa maswali haya ni: La! Je, mwanadamu yeyote, akiwemo Nuhu, anaweza kuthamini yale maumivu ambayo Mungu alikuwa akihisi wakati huo? Je, mtu yeyote anaweza kufahamu ni kwa nini Mungu alianzisha agano kama hilo? Hakuna anayeweza! Mwanadamu hathamini maumivu ya Mungu si kwa sababu hawezi kuelewa maumivu ya Mungu, na si kwa sababu ya nafasi iliyopo kati ya Mungu na mwanadamu au tofauti kati ya hadhi yao; badala yake, ni kwa sababu mwanadamu hata hajali kuhusu hisia zozote za Mungu. Mwanadamu anafikiria Mungu yuko huru—Mungu hahitaji watu wa kujali kuhusu Yeye, kumwelewa au kumwonyesha namna anavyomfikiria. Mungu ni Mungu, hivyo Hana maumivu, hana hisia; Hatakasirika, Hahisi huzuni, hata Halii. Mungu ni Mungu, hivyo Hahitaji maonyesho yoyote ya kihisia na Hahitaji faraja yoyote ya kihisia. Kama Hahitaji mambo haya katika hali fulani, basi ya Atatatua mwenyewe na Hatahitaji usaidizi wowote kutoka kwa mwanadamu. Lakini kinyume chake ni kuwa, ni wale binadamu wanyonge, wanaohitaji tulizo, toshelezo, himizo la Mungu na hata pia kwake Yeye kuweza kutuliza hisia zao wakati wowote mahali popote. Fikira kama hiyo inajificha ndani kabisa ya mioyo ya mwanadamu: Binadamu ndiye mnyonge; wanahitaji Mungu ili awatunze kwa kila njia, wanastahili utunzaji wote wanaopokea kutoka kwa Mungu, na wanafaa kudai kutoka kwa Mungu chochote kile wanachohisi kinafaa kuwa ni chao. Mungu ndiye mwenye Nguvu; Anacho kila kitu, na Anahitaji kuwa mlezi wa mwanadamu na Anayetoa baraka. Kwa sababu Yeye tayari ni Mungu, Yeye Mwenyezi na Hahitaji katu chochote kutoka kwa mwanadamu.
Kwa vile binadamu hatilii maanani ufunuo wowote wa Mungu, hajawahi kuhisi huzuni, maumivu au furaha ya Mungu. Lakini kinyume chake ni kwamba, Mungu anajua maonyesho yote ya binadamu kama vile anavyojua sehemu ya kiganja cha mkono Wake. Mungu hutosheleza mahitaji ya kila mtu siku zote na pahali pote, akiangalia fikira zinazobadilika za kila mmoja na hivyo basi kuwatuliza na kuwahimiza, na kuwaongoza na kuwaangazia. Kuhusu mambo yote ambayo Mungu amemfanyia mwanadamu, na gharama zote Alizolipia kwa sababu yao, watu wanaweza kupata kifungu kutoka kwa Biblia au kutoka kwa chochote ambacho Mungu amesema mpaka sasa kinachoelezea waziwazi kwamba Mungu atadai kitu kutoka kwa binadamu? La! Kinyume cha mambo, haijalishi ni vipiwatu wanapuuza kufikiria kwa Mungu, Bado Anawaongoza kwa marudio wanadamu, Anamkimu kwa kurudia mwanadamu na kumsaidia, kuwaruhusu kufuata njia za Mungu ili waweze kupokea hatima nzuri ambayo Amewatayarishia. Inapokuja kwa Mungu, kile Anacho na alicho, neema Yake, rehema Yake, na tuzo Zake zote, zitakabidhiwa bila ya kusita kwa wale wanaompenda na kumfuata Yeye. Lakini hajawahi kufichua kwa mtu yeyote maumivu aliyopitia Yeye au hali ya akili Yake, na katu halalamiki kuhusu yeyote ambaye hamtilii Yeye maanani au hajui mapenzi Yake. Anavumilia tu haya yote kimyakimya, akisubiria siku ambayo mwanadamu ataweza kuelewa.
Kwa nini Nasema mambo haya hapa? Ni nini mnachoona kutoka kwa mambo haya Niliyosema? Kuna kitu katika kiini na tabia ya Mungu ambacho ndicho rahisi zaidi kupuuza, kitu ambacho kinamilikiwa tu na Mungu na wala si mtu yeyote, wakiwemo wale wengine wanafikiria kwamba ni watu wakubwa, watu wazuri, au Mungu wa kufikiria kwao. Kitu hiki ni nini? Ni kule kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu. Tunapozungumzia kutokuwa na ubinafsi, unaweza kufikiria kwamba pia wewe huna ubinafsi, kwa sababu inapokuja kwa watoto wako, haujadiliani juu ya bei na wao na wewe ni mkarimu sana kwao, au unafikiria kwamba wewe huna ubinafsi sana inapokuja kwa wazazi wako. Haijalishi ni nini unafikiria, angaa unayo dhana ya neno “kutokuwa na ubinafsi” na unalifikiria kama neno zuri, na kwamba kuwa mtu asiye na ubinafsi ni jambo la kipekee. Wakati huna ubinafsi, unafikiri kuwa wewe ni mkubwa. Lakini hakuna mtu anayeweza kuona kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu miongoni mwa viumbe wote, miongoni mwa watu, hafla, na vitu, na kupitia kazi ya Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Kwa sababu binadamu ni mchoyo sana! Kwa nini Ninasema hivyo? Mwanadamu anaishi katika ulimwengu wa uyakinifu. Unaweza kumfuata Mungu, lakini huoni wala kushukuru namna ambavyo Mungu anakukimu, anavyokupenda na anavyoonyesha kwamba anakujali. Kwa hivyo unaona nini? Unaona watu wako wa ukoo wanaokupenda au kukupenda sana. Unayaona mambo ambayo ni ya manufaa kwa mwili wako, unajali kuhusu watu na vitu unavyopenda. Huku ndiko kutokuwa na ubinafsi kwa binadamu kunakodaiwa. Watu kama hao “wasiokuwa na ubinafsi” hata hivyo, huwa hawajali katu kuhusu Mungu anayewapa maisha. Kinyume na Mungu, kutokuwa na ubinafsi kwa binadamu kunakuwa cha ubinafsi na yenye uchoyo. Kutokuwa na ubinafsi ambako binadamu anasadiki katika ni ulio mtupu na usio wa kihalisia, uliotiwa madoa, usiolingana na Mungu, na usiohusika na Mungu. Kutokuwa na ubinafsi kwa binadamu ni kwa ajili yake, huku kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu ni ufunuo wa kweli wa kiini Chake. Ndipo hasa kutokana na kujitolea nafsi kwa Mungu ndipo binadamu anapokea ufululizo usiosita wa ujazo kutoka kwake. Huenda msiathirike sana na mada hii Ninayozungumzia kuhusu leo na unaweza kuwa tu unatikisa kichwa chako kwa kukubaliana nami, lakini wakati unapojaribu kufurahia moyo wa Mungu katika moyo wako, utaweza kwa kutojua kugundua: Miongoni mwa watu wote, masuala, na mambo unaweza kuhisi katika ulimwengu huu ni kutokuwa na ubinafsi tu kwa Mungu ambako ni kweli na dhabiti, kwa sababu ni upendo wa Mungu tu kwako ndio ambao hauna masharti na hauna madoa. Bali na Mungu, kutokuwa na kile kinachodaiwa kutokuwa na ubinafsi wa mtu mwengine ni bandia, cha juujuu, kisicho na msingi; kina kusudio, nia fulani, kinatekeleza shughuli ya masikilizano,na hakiwezi kupimwa kamwe. Mnaweza hata kusema kwamba ni ki chafu, na cha kudharauliwa. Je, mnakubali?
Ninajua hamjazoeana na mada hizi na mnahitaji muda kidogo ili ziweze kuingia ndani yenu kabla mnaweza kuelewa kwa kweli. Kwa kadri mnavyokuwa kwamba hamjazoeana na masuala na mada hizi, ndipo inapothibitisha zaidi kwamba mada hizi zinakosekana katika mioyo yenu. Kama Singetaja mada hizi, yupo yeyote kati yenu ambaye angeweza kujua kidogo kuzihusu? Nasadiki hamngewahi pata kuyajua. Hii ni ya hakika. Haijalishi ni kiasi kipi mnachoweza kufahamu au kuelewa, kwa ufupi, mada hizi Ninayozungumzia ndizo ambazo watu wanakosa sanasana na wanazofaa kujua kuhusu zaidi. Mada hizi ni muhimu kwa kila mmoja—ni zenye thamani na ndiyo maisha, na ni mambo ambayo lazima mmiliki vizuri kwa safari ijayo. Bila ya maneno haya kama mwongozo, bila ya uelewa wako wa tabia ya Mungu na kiini, siku zote utabakia na alama ya kiulizio inapokuja kwa Mungu. Unawezaje kusadiki kwa Mungu kwa njia bora kama hata humwelewi Yeye? Hujui chochote kuhusu hisia Zake, mapenzi Yake, hali ya akili Yake, kile Anachofikiria, nini kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni, na nini kinachomfanya Yeye kuwa na furaha, hivyo unawezaje kuweka moyo wa Mungu katika fikira?
Kila wakati Mungu anapokuwa amekasirika, Anakumbana na mwanadamu ambaye hamtilia maanani kamwe, mwanadamu anayemfuata Yeye na anayedai kumpenda Yeye lakini anapuuza kabisa hisia Zake. Moyo Wake utakosaje kuumia? Katika kazi ya usimamizi ya Mungu, Anaitekeleza kwa dhati kazi Yake na Anaongea na kila mmoja Anawatazama bila kizuizi chochote au kujificha, lakini kinyume chake ni kuwa, kila mtu anayemfuata Yeye anatenganishwa na Yeye, na hakuna aliyeradhi kujishughulisha na kuwa karibu na Yeye, kuelewa moyo Wake, au kutilia maanani hisia Zake. Hata wale wanaotaka kuwa wandani wa Mungu hawataki kuwa karibu na Yeye, kutilia maanani moyo Wake, au kujaribu kumwelewa Yeye. Wakati Mungu anashangilia na ana furaha, hakuna yeyote yule wa kushiriki katika furaha hiyo na Yeye. Wakati Mungu anakosa kueleweka na watu, hakuna mtu wa kutuliza moyo Wake ulio na majeraha. Wakati moyo Wake unaumia, hakuna hata mtu mmoja aliye radhi kumsikiliza Yeye na kuwa mwandani Wake. Katika hii maelfu ya miaka ya usimamizi wa kazi ya Mungu, hakuna mtu anayeelewa hisia za Mungu, hakuna hata mtu anayefahamu au kutambua hisia Zake, tupilia mbali hata yeyote ambaye angesimama kando ya Mungu ili kushiriki katika furaha na huzuni Zake. Mungu ni mpweke. Yeye ni pweke! Mungu ni mpweke si tu kwa sababu wanadamu waliopotoka wanampinga Yeye, lakini zaidi kwa sababu wale wanaofwatilia kuwa wa kiroho, wale wanaotafuta kumjua Mungu na kumwelewa Yeye, na hata wale walioradhi kujitolea maisha yao yote kwake Yeye, pia hawajui fikira Zake, na hawaielewi tabia Yake na hisia Zake.
Mwishoni mwa hadithi ya Nuhu, tunaona kwamba Mungu alitumia mbinu isiyo ya kawaida kuelezea hisia Zake wakati huo. Mbinu hii ni maalumu sana, na ni kuweka agano na binadamu. Ni mbinu inayotangaza mwisho wa matumizi ya gharika na Mungu katika kuangamiza ulimwengu. Kutoka nje, kuweka agano kunaonekana kuwa jambo lililo la kawaida sana. Si jambo lolote zaidi ya kutumia maneno kufunga wahusika ili wasitende vitendo vitakavyokiuka agano, ili kusaidia kutimiza kusudio la kulinda maslahi ya pande zote mbili. Kwa umbo, ni jambo la kawaida sana, lakini kutoka kwa motisha zilizopo na maana ya Mungu kufanya kitu hiki, ni ufunuo wa kweli wa tabia ya Mungu na hali Yake ya akili. Endapo utayaweka maneno haya kando na kuyapuuza, kama Sitawahi kukuambia ukweli wa mambo, basi ubinadamu hautawahi kwa hakika kujua kufikiria kwa Mungu. Pengine katika kufikiria kwako Mungu anatabasamu wakati anapofanya agano hili, au pengine maonyesho Yake ni ya kumakinika, lakini haijalishi ni aina gani iliyo maarufu zaidi ya maonyesho Aliyonayo Mungu katika kufikiria kwa watu, hakuna mtu anayeweza kuona moyo wa Mungu au maumivu Yake, na hata upweke Wake. Hakuna mtu anayeweza kumfanya Mungu kumwamini au anayestahili kuaminiwa na Mungu, au kuwa mtu Anayeweza kueleza fikira Zake au kuwa mwandani Wake wa kuambia maumivu Yake. Ndiyo maana Mungu hakuwa na chaguo ila kufanya kitu kama hicho. Kwa juujuu, Mungu alifanya jambo rahisi la kuuaga ubinadamu ule wa awali, kuhitimisha hali ya kale ilivyokuwa na kufikia hitimisho halisi katika kuangamiza Kwake kwa ulimwengu akitumia gharika. Hata hivyo, Mungu alikuwa ameyazika maumivu kutoka muda huu ndani kabisa ya moyo Wake. Kwa wakati ambao Mungu hakuwa na yeyote wa kuita mwandani, aliunda agano na wanadamu, akiwaambia kwamba asingeuangamiza ulimwengu kwa gharika tena. Wakati upinde wa mvua unapojitokeza ni kukumbusha watu kwamba, kitu kama hicho kiliwahi kufanyika, kuwapa onyo watu dhidi ya kufanya maovu. Hata katika hali hiyo ya maumivu, Mungu hakusahau kuwahusu wanadamu na bado akaonyesha kujali kwingi sana kwao. Je, huu si upendo na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu? Lakini nao watu wanafikiria nini wakati wanapoteseka? Kwani huu si wakati ambao wanamwitaji Mungu zaidi? Katika nyakati kama hizi, siku zote watu humkokota Mungu katika mambo yao ili Mungu aweze kuwapa tulizo. Haijhalishi ni lini, Mungu hatawahi kuwavunja moyo watu wake, na siku zote Atawaruhusu watu kutoka katika changamoto zao na kuishi katika mwangaza. Ingawaje Mungu anawakimu wanadamu, ndani wa moyo wa binadamu, Mungu si chochote wala lolote ila tembe ya kumhakikishia tu mambo, dawa ya tulizo. Wakati Mungu anateseka, wakati moyo Wake una majeraha, kuwa na kiumbe aliyeumba au mtu yeyote wa kuwa mwandani wake au wa kumtuliza Yeye kwa kweli kwake Mungu ni tamanio tu la kibadhirifu asiloweza kutegemea. Siku zote binadamu hatilii maanani hisia za Mungu, hivyo Mungu siku zote haulizii wala hatarajii kuwa kuna mtu anayeweza kumtuliza Yeye. Anatumia mbinu Zake mwenyewe kueleza hali Yake. Watu hawafikirii kwamba ni jambo kubwa kwa Mungu kupitia mateso fulani, lakini unapojaribu tu kuelewa Mungu kwa kweli, unapoweza kushukuru kwa dhati, nia nzuri za Mungu katika kila kitu anachofanya, ndipo unapoweza kuhisi ukubwa wa Mungu na kutokuwa na ubinafsi kwake. Ingawaje Mungu aliunda agano na wanadamu kutumia upinde wa mvua, hakuwahi kuambia yeyote kwa nini alifanya hivi, kwa nini alianzisha agano hili, kumaanisha hakuwahi kuambia mtu fikira Zake halisi. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufahamu kina cha upendo ambao Mungu anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake mwenyewe, na hakuna pia mtu anayeweza kutambua ni kiasi kipi cha maumivu moyo Wake uliteseka wakati Alipouangamiza ubinadamu. Hivyo basi, hata kama Angeambia watu namna Anavyohisi, hawawezi kumwamini. Licha ya kuwa katika maumivu, angali Anaendelea na hatua inayofuata ya kazi Yake. Siku zote Mungu Anautoa upande wake bora zaidi na mambo bora zaidi kwa wanadamu huku yeye Mwenyewe Akistahimili kimyakimya mateso yote. Mungu kamwe hafichui mateso haya. Badala yake, Anayavumilia na kusubiri kwa kimya. Ustahimilivu wa Mungu si wa kimya tu, usio na hisia, au usio na suluhu, wala si ishara ya unyonge. Ni kwamba upendo na kiini cha Mungu siku zote yamekuwa bila ubinafsi. Huu ni ufunuo wa kiasili wa kiini na tabia Yake na maonyesho halisi wa utambulisho wa Mungu kama Muumba wa kweli.
Baada ya kusema hayo, baadhi ya watu wanaweza kufasili vibaya kile Ninachomaanisha. Je kufafanua hisia za Mungu kwa maelezo kama hayo, kwa hali ya hisia nyingi sana, inanuia kuwafanya watu kuhisi masikitiko kwa Mungu. Kulikuwa na nia kama hilo? (La!) Kusudio la pekee la mimi kusema maneno haya ni kuwafanya kujua Mungu kwa njia bora zaidi, kuelewa kila sehemu Yake, kuelewa hisia Zake, kutambua kiini na tabia ya Mungu , kwa uthabitu na kwa kidogo kidogo, iliyoelezewa kupitia kwa kazi Yake, kinyume na vile inavyotumiwa kupitia kwa maneno matupu ya binadamu, barua na mafundisho yao ya kidini,, au kufikiria kwao. Hivi ni kusema, Mungu na kiini cha Mungu kwa kweli vipo—si tu uchoraji, havijafikiriwa, havijajengwa na binadamu, na bila shaka havijabuniwa na wao. Je, mnatambua hii sasa? Kama mnaitambua, basi maneno Yangu leo yametimiza shabaha yao.
Tulizungumzia mada tatu leo. Nina imani kila mmoja amepata pakubwa kutoka kwenye ushirika huu kuhusu mada hizi tatu. Ninaweza kusema kwa hakika kwamba, kupitia kwa mada hizi tatu, fikira za Mungu Nilizofafanua au kiini cha Mungu Nilichotaja vyote vimeweza kugeuza fikira na uelewa wa watu kuhusu Mungu, na hata kupindua imani za kila mmoja kwa Mungu, na zaidi, kupindua picha ya Mungu inayopendwa na kila mmoja katika mioyo yao. Haijalishi ni nini, Natumai kwamba kile mmejifunza kuhusu tabia ya Mungu katika sehemu hizi mbili za Biblia ni cha manufaa kwenu, na Natumai kwamba baada ya nyinyi kurudi mtajaribu kukitafakari zaidi. Kikao cha leo kinahitimishwa hapa. Kwaheri!

Mei 18, 2014

kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi? 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni