Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja
Ni wakati tu ambapo Mungu huanza kunena na kutenda ndipo watu humfahamu Yeye kidogo katika dhana zao. Hapo mwanzo, ufahamu huu huwepo tu ndani ya dhana zao, lakini kadiri muda unavyopita, watu huanza kuhisi kwamba mawazo yao wenyewe yanaendelea kutokuwa na manufaa na hayafai; hivyo, wao huja kuamini yote ambayo Mungu husema, kiasi kwamba wao "hutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya akili zao.” Ni katika akili zao pekee ndipo watu huwa na mahali pa Mungu wa vitendo.