Utambulisho
Mpaka siku moja,
utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena,
kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako,
kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako,
kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo,
kwamba Muumba siye Yule unayemtamania katika mawazo yako
lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako,
kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako,
Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako, kudhibiti majaliwa yako.
Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni.
Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako,
Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.