Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli.


