"Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka katika macho yao; na hakutakuwa na kifo tena, wala uchungu, wala kilio, wala hakutakuwa na maumivu tena; maana ile hali ya kale imepita!"(Ufunuo 21:4)
(Ufunuo 21:3) "Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao."
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi.
Swahili Gospel Song Video "Shukrani na Sifa kwa Mwenyezi Mungu" | God Guided Me to a New Life
Utambulisho
I Tumeletwa mbele ya Mungu. Maneno Yake tunakula na kunywa. Roho Mtakatifu anatupa nuru, tunaelewa ukweli anaonena Mungu. Mila za dini, tumezitupa, minyororo yote. Isiyozuiliwa na sheria, mioyo yetu inawekwa huru. Na sisi tunafurahi iwezekanavyo, tukiishi katika nuru ya Mungu, kufurahi iwezekanavyo, kuishi katika nuru ya Mungu.
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli.
Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya
Nyote mmeshuhudia wenyewe kazi ambayo Nimefanya miongoni mwenu, ninyi wenyewe mmesikia maneno ambayo Nimenena, nanyi mnajua mtazamo Wangu kuelekea kwenu, kwa hiyo mnapaswa kujua kwa nini Ninafanya kazi hii miongoni mwenu. Nitawaambia ukweli—ninyi ni vifaa tu vya kazi Yangu ya ushindi katika siku za mwisho; ninyi ni vyombo vya kupanua kazi Yangu miongoni mwa nchi za Mataifa.