9/27/2018

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki



Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Utambulisho

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

9/26/2018

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God



Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God


Utambulisho

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.

9/25/2018

Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?



Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?


Utambulisho

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. … Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria."
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

9/24/2018

9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Zhang Min, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mvua ilianza kunyesha sana asubuhi. Kufikia wakati wa adhuhuri wakati nilipaswa kwenda kwa mkutano, niliona mvua ilikuwa nzito sana kiasi kwamba sikutaka kwenda. Lakini ulikuwa mara moja tu kwa wiki, kama singeenda singekuwa na njia yoyote ya kufanya kazi yangu ya kanisa. Chochote kilichokuwako kikiendelea nje, bado ilinipasa nishiriki nao. Nilipofikiria hayo, niliharakisha kwenda kwa mkutano. Baada ya saa kumi alasiri hiyo, yule ndugu wa kiume wa mahali pa kukutana alikimbia akarudi nyumbani akisema: "Bado mnafanya mkutano, endeni nyumbani, kuna maji mengi yanayoteremka pale." Nilikwenda na kuangalia na kulikuwa na maji mengi sana yaliyokuwa yakiteremka, mto huo ulikuwa umefurika na ukipanda juu sana.

9/23/2018

Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?



Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?


Utambulisho

Wokovu ni nini? Wale wanaoamini katika Bwana Yesu hufikiria kwamba ikiwa wataomba kwa dhati kwa Bwana, waungame dhambi zao, na kutubu, dhambi zao zitasamehewa, na watapewa wokovu, na Bwana Atakapokuja, wao watainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini je, wokovu kweli ni rahisi hivyo?

9/22/2018

7. Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

7. Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

Li Jing, Beijing
7 Agosti, mwaka wa 2012
Siku hiyo, ilianza kunyesha asubuhi. Nilikwenda kwa mkutano nyumbani mwa ndugu mmoja, wakati mvua ilipoendelea kuongezeka zaidi na zaidi kwa uzito. Kufikia alasiri ilikuwa ikinyesha kana kwamba ilitoka mbinguni moja kwa moja. Wakati tulipomaliza mkutano wetu, mvua ilikuwa imeingia katika ua wa ndugu yangu, lakini kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya familia yangu, nilijitahidi kwenda nyumbani.

9/21/2018

41. Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

41. Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Siqiu   Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang
Wakati wowote ninapoona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu, “Ikiwa daima umekuwa mwaminifu Kwangu na kunipenda, lakini unapitia mateso ya maradhi, misukosuko ya maisha, na kutelekezwa na marafiki na jamaa au kupitia maafa mengine yoyote maishani, basi, uaminifu na mapenzi yako Kwangu yataendelea kuwepo?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ninahisi hasa bila furaha—hisi ya huzuni hunyatia ndani yangu na moyo wangu husema malalamiko yake yasiyoghuna: Ewe Mungu, Unawezaje kuruhusu wale walio waaminifu Kwako na wanaokupenda Wewe kukutana na msiba wa jinsi hiyo?