10/02/2018

Swahili Christian Skit | "Polisi Waenda kwa Ziara ya Mwaka Mpya" (Kichekesho)



Swahili Christian Skit | "Polisi Waenda kwa Ziara ya Mwaka Mpya" (Kichekesho)


Utambulisho

Zheng Xinming, mwanamume mzee wa karibu miaka sabini, ni Mkristo wa dhati. Kwa sababu ya imani yake katika Bwana, aliwekwa kizuizini na kufungwa gerezani, na kuhukumiwa miaka nane. Alipoachiliwa, bado alikuwa ameorodheshwa na Polisi wa Kikomunisti wa China kama mlengwa wa ufuatiliaji wa kuzingatiwa. Hasa, baada ya mzee huyo kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, polisi walikuja karibu kila siku kumtisha, kumuogofya na kumsumbua. Hakukuwa na njia ya Zheng Xinming kusoma neno la Mungu nyumbani kwa kawaida, na hata familia yake ilishiriki hali yake ya wasiwasi. Sasa ni Mkesha wa Mwaka Mpya na mzee yuko nyumbani akisoma neno la Mungu, bila kujua nini kinaweza kutokea …

Yaliyopendekezwa: Asili ya Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

10/01/2018

Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

10. Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

Wenzhong , Beijing
Agosti 11, mwaka wa 2012
Usiku wa Julai 21, mwaka wa 2012, tulikuwa na mafuriko makubwa hapa, ambayo hutokea kwa nadra. Ningependa kumwambia kila mtu aliye na kiu ya Mungu kile nilichokipitia kwa kweli na kukiona wakati huo.
Siku hiyo mume wangu nami tuliutunza uga wa chakula kikavu cha mifugo wa dada yangu. Wakati wa usiku mvua nzito iliendelea kunyesha, na tulienda kulala mapema sana.

9/30/2018

95. Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

95. Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

Mo Zhijian Mkoa wa Guangdong
Nilizaliwa katika eneo maskini, la mbali lenye milima ambako tumefukiza na kumwabudu Budha kwa vizazi vingi. Kuna hekalu za Budha sehemu hiyo kote ambako familia zote zingekwenda kuchoma uvumba; hakuna mtu yeyote aliyewahi kumwamini Mungu kamwe. Katika mwaka wa 1995, mimi na mke wangu tulikuwa katika sehemu nyingine ya nchi ambapo tulimwamini Bwana Yesu; baada ya sisi kurudi tulianza kushiriki injili na idadi ya watu ambao waliikubali ilikua polepole hadi watu zaidi ya 100. Kwa sababu watu zaidi na zaidi walikuwa wakimwamini Mungu, liliishtua serikali ya mitaa.

9/29/2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?



Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?


Utambulisho

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini hufuata unabii unaosema kwamba Bwana atashuka akiwa juu ya wingu na wanamsubiria Yeye kuja kwa njia hiyo kisha kuwanyakua hadi kwenye ufalme wa mbinguni, lakini wanapuuza unabii mbalimbali wa Bwana kuhusu kuja kwa siri: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Hivyo unabii huu mbalimbali wa kurudi kwa Bwana unatimizwa vipi? Na tunafaa kuwa vipi wanawali wenye hekima ambao wanakaribisha kurudi kwa Bwana?
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

9/28/2018

Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Momo     Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui
Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, “Hakuna maumivu, hakuna faida,” na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu. Wakati Mungu alinifichulia ukweli, hatimaye niligundua kuwa nilikuwa nikiishi chini ya jozi la Shetani, nikiishi chini ya miliki yake.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Ushuhuda, Umeme wa Mashariki

9/27/2018

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki



Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Utambulisho

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

9/26/2018

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God



Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God


Utambulisho

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.