Utambulisho
Mwenyezi Mungu anasema, "Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini.