Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu
Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Ruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima
Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu wa mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye— ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu.
Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemekana kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.
Onyo na Upataji Nuru Ulilotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu
Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumpeleka Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua upya umuhimu wake. Hawawi na wasiwasi tena kuhusu kama wao wenyewe watapitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi tena au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
...
...
Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni