Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea.
Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au ndugu wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali kwa mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu.