5/07/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 43


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 43

Je, Sijawakumbusha? Msiwe wenye hofu; ninyi hamjanisikiliza tu, watu wasio na fikira ninyi! Je, mtaweza kuuelewa moyo Wangu lini? Kila siku kuna nuru mpya, kila siku kuna mwanga mpya. Ni mara ngapi mmeuelewa kwa ajili yenu wenyewe? Je, Sijawaambia Mwenyewe? Bado ninyi ni wa kukaa tu kama wadudu ambao watasonga tu wanaposukumwa, lakini hamwezi kuchukua hatua ya kushirikiana na Mimi, kuufikiria mzigo Wangu.

5/06/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 42

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 42

Jinsi gani matendo ya Mwenyezi Mungu yalivyo makuu! Jinsi ilivyo ya ajabu! Jinsi ilivyo ya kushangaza! Tarumbeta saba zinatoa sauti, ngurumo saba zinatolewa, bakuli saba zinamwangwa—hii itadhihirika wazi mara moja na hakuwezi kuwa na shaka. Upendo wa Mungu huja juu yetu kila siku na ni Mwenyezi Mungu pekee Anayeweza kutuokoa; kama tunakabiliwa na bahati mbaya au kupokea baraka ni kwa sababu Yake kabisa, na sisi wanadamu hatuna njia ya kuamua hili.

5/05/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 41

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi.

5/04/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 40

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 40

Kwa nini ninyi ni wa mwendo wa polepole? Kwa nini hamsikii? Makumbusho kadhaa hayajawazindua; hili linanihuzunisha. Kwa kweli Sipendi kuwaona wanangu namna hii. Moyo Wangu unawezaje kustahimili hili? Ah! Lazima Niwafundishe kwa mkono Wangu mwenyewe. Mwendo Wangu unaendelea kuwa wa kasi. Wanangu! Inukeni haraka na mshirikiane na Mimi. Nani wanajitumia kwa dhati kwa ajili Yangu sasa?

5/03/2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

5/02/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 39

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 39

Fungua macho yako na uangalie na unaweza kuona nguvu Zangu kuu kila mahali! Unaweza kuwa na uhakika na Mimi kila mahali. Ulimwengu na anga unaeneza nguvu Zangu kuu. Maneno ambayo Nimenena yametimia katika ongezeko la joto la hali ya hewa, mabadiliko ya hali ya hewa, vioja vya watu, ulemavu wa elimumwendo ya kijamii, na udanganyifu wa mioyo ya watu. Jua linakuwa jeupe na mwezi unakuwa mwekundu; Yote yako katika machafuko. Je, bado huoni haya?

5/01/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 38

Sauti ya Mungu  | Sura ya 38 

Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme! Lazima uelewe kwamba kile kinachofanywa[a] leo ni kazi ya ajabu ya Mungu; hakina uhusiano na mwanadamu.