6/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi Yangu yote ni maonyesho ya mapenzi Yangu. Ni nani anayeweza kuudhukuru mzigo Wangu? Nani anayeweza kuelewa nia Yangu? Je, mmefikiria kila moja ya maswali Niliyoibua kwenu? Uzembe ulioje! Unathubutu vipi kuvuruga mipango Yangu? Wewe u mshenzi kweli! Kazi kama hii ya pepo wabaya ikiendelea, Nitawatupa mautini mara moja katika shimo lisilo na mwisho! Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya.

6/15/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75
Yote yatatimizwa punde tu maneno Yangu yanapozungumzwa, bila kupotoka hata kidogo. Kuanzia sasa kwendelea, mafumbo yote yaliyofichwa hayatazuiwa au kufunikwa hata kidogo, na yatafichuliwa kwenu—wanangu wapendwa. Nitakufanya uone hata ishara na maajabu kubwa zaidi ndani Yangu, na kuona hata mafumbo makubwa zaidi. Mambo haya hakika yatawashangaza na kuwapa ufahamu bora zaidi wa Mimi, mwenyezi Mungu, na kuwaruhusu kufahamu hekima Yangu humo.

6/14/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 74

Sauti ya Mungu | Sura ya 74

Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija juu yako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa tena na huzuni na hakutakuwa na machozi?

6/13/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 73

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 73

Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu. Ni ya kutaka uangalifu mkubwa hasa.

6/12/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha.

6/11/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Sharti unitegemee kuondoa upungufu ama udhaifu mara tu unapougundua. Usichelewe; vinginevyo kazi ya Roho Mtakatifu atakuwa mbali sana nawe, na utaanguka nyuma mbali sana. Kazi ambayo Nimekuaminia inaweza kutimizwa kwa kupitia tu kukaribia kwako mara kwa mara, kuomba, na kuwa na ushirika katika uwepo Wangu. Kama sivyo, hakuna matokeo yoyote yatakayofikiwa, na kila kitu kitakuwa bure. Kazi Yangu leo si kama ilivyokuwa awali. Kadiri ya maisha kwa watu Ninaowapenda si kama ilivyokuwa mbeleni.

6/10/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 71

Maneno ya Mungu | Sura ya 71

Mimi wote Nimejiweka dhahiri kwenu, lakini kwa nini mnashindwa kutafakari maneno Yangu kwa mioyo na nafsi zenu zote? Kwa nini mnachukua maneno Yangu kama takataka? Je,yote Ninayosema ni makosefu? Je, maneno Yangu yamekupiga katika sehemu ya uzima? Daima kuchelewesha, daima kusita, kwa nini mnafanya mambo hivi? Je, Mimi sijaongea wazi?