6/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Vipofu! Wajinga! Rundo la takataka lisilo na maana! Nyinyi hutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu! Je, hamfikiri kuwa hii ni dhambi dhidi Yangu? Na zaidi ni kuwa ni kitu ambacho ni vigumu kusamehe! Mungu wa vitendo anakuja miongoni mwenu leo lakini mwajua tu upande Wangu mmoja ambao ni ubinaamu Wangu wa kawaida, na hamjaona kabisa upande Wangu ambao ni wa kiungu kabisa. Je, unafikiri kuwa Sijui anayejaribu kunidanganya kisirisiri?

6/20/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 78

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 78
Nimesema kabla ya kuwa kazi inafanywa na Mimi, sio na mwanadamu yeyote. Kwangu, kila kitu kimetulia na kufurahi, lakini na ninyi mambo ni tofauti sana na chochote mnachofanya ni kigumu sana. Kitu chochote Ninachokubali hakika kitatimizwa na Mimi, wakati mtu yeyote Ninayemkubali atakamilishwa na Mimi. Wanadamu—msiingilie katika kazi Yangu! Chote tu mnachohitaji kujishughulisha nacho ni kufuata uongozi Wangu, kufanya kile Ninachopenda, kukataa yote ambayo Ninayachukia, mjivute kutoka kwa dhambi, na mjitupe ndani ya kumbatio Langu lenye upendo.

6/19/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?

6/18/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi.

6/17/2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu.

6/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi Yangu yote ni maonyesho ya mapenzi Yangu. Ni nani anayeweza kuudhukuru mzigo Wangu? Nani anayeweza kuelewa nia Yangu? Je, mmefikiria kila moja ya maswali Niliyoibua kwenu? Uzembe ulioje! Unathubutu vipi kuvuruga mipango Yangu? Wewe u mshenzi kweli! Kazi kama hii ya pepo wabaya ikiendelea, Nitawatupa mautini mara moja katika shimo lisilo na mwisho! Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya.

6/15/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75
Yote yatatimizwa punde tu maneno Yangu yanapozungumzwa, bila kupotoka hata kidogo. Kuanzia sasa kwendelea, mafumbo yote yaliyofichwa hayatazuiwa au kufunikwa hata kidogo, na yatafichuliwa kwenu—wanangu wapendwa. Nitakufanya uone hata ishara na maajabu kubwa zaidi ndani Yangu, na kuona hata mafumbo makubwa zaidi. Mambo haya hakika yatawashangaza na kuwapa ufahamu bora zaidi wa Mimi, mwenyezi Mungu, na kuwaruhusu kufahamu hekima Yangu humo.