10/04/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa



Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele.  Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu?

10/01/2019

Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili



"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili


Mwenyezi Mungu anasema, “Maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia, na upanga mkali ukatao kuwili, ambao unaweza kumshinda Shetani” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ni kama upanga wenye makali pande mbili, yanayoweza kushinda nguvu zote za uovu. Je, umepitia nguvu na mamlaka ya kutisha ya maneno ya Mungu?

Tazama Zaidi: Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"

9/28/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 111


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 111


Mataifa yote yatabarikiwa kwa sababu Yako; watu wote watanikaribisha kwa shangwe na kunisifu kwa sababu Yako. Ufalme Wangu utafanikiwa na kukua, na utabaki milele. Hakuna mtu ataruhusiwa kuukanyaga na hakuna kitu kitaruhusiwa kuwepo ambacho hakikubaliani na Mimi, kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye uadhama na asiyekosewa Mwenyewe. Sikubali mtu yeyote anihukumu na Sikubali mtu yeyote kutolingana na Mimi. Hili linatosha kuonyesha tabia Yangu na uadhama Wangu.

9/25/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 110

Sauti ya Mungu | Sura ya 110


Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.

9/22/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 109


Maneno ya Mungu | Sura ya 109


Ninatoa matamko kila siku, kuzungumza kila siku, na kufichua ishara Zangu kuu na shani kila siku. Haya yote ni kazi ya Roho Wangu. Machoni pa watu Mimi ni mwanadamu tu, lakini hasa ni katika mwanadamu huyu ndipo Ninafichua vyote Vyangu na nguvu Yangu kuu.

Kwa kuwa watu humpuuza mwanadamu Niliye na huyapuuza matendo Yangu, wanafikiri kuwa hivi ni vitu ambavyo hufanywa na wanadamu. Lakini mbona hufikiri: Je, watu wanaweza kutimiza yale Ninayoyatenda? 

9/19/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108


Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa. Watu hawa wanaitwa wafu wasio na roho. Nami Nawaita wale walio ndani Yangu watu walio hai wenye roho. Wao ni Wangu, na watarudi kwenye kiti Changu cha enzi. Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo.

9/16/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”


Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”


Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu?