6/08/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Kisha, hebu tuangalie kile Mungu alimfanyia Ibrahimu. Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: “Naye akasema, Umchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, uende mpaka nchi ya Moria; na huko umtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo Nitakaokuambia.” Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa minajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kupata mtoto, Mungu alimwomba amtoe mwana wake—haiwezekani! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio halisi la Mungu lilikuwa nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Katika mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya “kuunda tatizo pasipo na tatizo” Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji mengi sana. Ingawaje alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: “Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda hadi mahali alipoambiwa na Mungu.” (Mwa 22:3). “Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu; Abrahamu akajenga madhabahu huko, akazipanga kuni tayari, na akamfunga Isaka mwanawe, na akamweka juu ya madhabahu juu ya zile kuni. Abrahamu akanyosha mkono wake, akakichukua kisu ili amchinje mwanawe.” (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake, na kukichukua kisu ili kumwua mtoto wake, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili kumwua mtoto wake—hilo lilionyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu—utiifu uleule ambao Yeye Alitamani.
Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kupangilia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni ukosefu wa mwafaka huu na kutofahamu ndiyo majaribio ya Mungu na mtihani wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kushibisha mahitaji ya Mungu. Hapo tu, wakati Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na Mungu—kwa Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na hakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawaje lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi furaha, Alihisi upendo wa binadamu kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati huu ambao Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili kumwua Isaka, Mungu alimsimamisha? Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumpa Isaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Yaweza kusemekana kwamba matokeo haya yalimtosheleza Mungu na kwamba ndiyo ambayo Mungu alitaka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawaje, katika miktadha tofauti, Mungu anatumia njia tofauti za kupima kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya “kutokuwa na masharti” ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeachana na ile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii yaonyesha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado hajapata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumuua mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Ni jambo la kiasili, hivyo basi, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli? Tutaachia hapa kwa mada hii. Halafu, tutasoma “Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.”
3. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu
(Mwa 22:16-18) … Nimeapa kwa nafsi yangu, akasema BWANA, kwa kuwa umetenda jambo hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee: Kwamba katika kubariki Nitakubariki, na katika kuzidisha Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulio kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa; kwa sababu umeitii sauti yangu.
Huu ni ukamilifu wa maelezo ya baraka za Mungu kwa Ibrahimu. Ingawaje ni fupi, maudhui yake ni mengi: Yanajumuisha sababu ya, na usuli wa, zawadi ya Mungu kwa Ibrahimu, na kile ambacho Alimpa Ibrahimu. Unao pia mhemko wa furaha na msisimko Aliotumia Mungu kutamka maneno haya, , pamoja na udharura wa tamanio Lake la kupata wale wanaoweza kusikiliza maneno Yake. Katika haya, tunaona upendo wa Mungu kwa, na wema Wake kwa, wale wanaotii maneno Yake na kufuata amri Zake. Hivyo, pia, tunaiona gharama Anayolipia ili kupata watu, na utunzaji na fikira Anazotumia kuweza kuwapata. Zaidi ya hayo, kifungu hicho, kilicho na maneno “Nimeapa kwa nafsi yangu,” kinatupa hali ya nguvu ya machungu na maumivu Aliyoyapitia Mungu, na Mungu pekee, usiri wa kazi hii ya mpango wa usimamizi. Ni kifungu cha kuchokonoa fikira, na kile ambacho kilikuwa na umuhimu maalum kwa, na ilikuwa na athari nyingi ajabu kwa wale waliokuja baadaye.

Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II 

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni