Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake
Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake
Je, baraka aliyopewa Ibrahimu na Mungu tuliyoisoma hapa ni kubwa? Ilikuwa kubwa vipi? Kunayo sentensi moja muhimu hapa: “na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa,” ambayo inaonyesha kwamba Ibrahimu alizipokea baraka ambazo hazikupewa tena kwa mwingine aliyekuja kabla au baadaye.
Wakati, alipoulizwa na Mungu, Ibrahimu alimrudisha mwana wake wa pekee—mtoto wake pekee wa kiume na mpendwa Isaka—kwa Mungu (dokezo: Hapa hatuwezi kutumia neno “tolewa sadaka”; tunafaa kusema alimrudisha mtoto wake kwa Mungu), Mungu naye hakumruhusu tu Ibrahimu kutoa Isaka, lakini pia Alimbariki. Ni kwa ahadi gani Alimbariki Ibrahimu? Ahadi ya kuzidisha watoto wake. Na walizidishwa mara ngapi? Maandiko yanatuelezea rekodi hii: “kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulio kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa.” Mungu Aliyatamka maneno haya katika muktadha upi? Hivi ni kusema, ni vipi ambavyo Ibrahimu alipokea baraka za Mungu? Alizipokea kama vile tu Mungu anavyosema kwenye maandiko: “kwa sababu umeitii sauti yangu.” Yaani, kwa sababu Ibrahimu alikuwa amefuata amri ya Mungu, kwa sababu alikuwa amefanya kila kitu ambacho Mungu alikuwa amesema, kuomba na kuamuru bila ya malalamiko hata kidogo, hivyo Mungu akatoa ahadi hiyo kwake. Kunayo sentensi moja muhimu katika ahadi hii ambayo inagusia fikira za Mungu wakati huo. Je, umeiona? Huenda hukutilia maanani sana maneno ya Mungu kwamba “Nimeapa kwa nafsi Yangu.” Yale yanamaanisha ni kwamba, wakati Mungu alipoyatamka maneno haya, Alikuwa anajiapisha Mwenyewe. Watu huapa kwa yapi wakati wanapokula kiapo? Wanaapa kwa Mbingu, hivi ni kusema, wanakula kiapo na jina la Mungu na kuapa kwa jina la Mungu. Huenda watu wasiwe na uelewa mwingi wa hali hiyo ambayo Mungu Alijiapisha mwenyewe, lakini mtaweza kuelewa Nitakapowapatia maelezo sahihi. Kukabiliwa na mtu ambaye aliweza tu kuyasikia maneno Yake lakini kutoelewa moyo Wake kwa mara nyingine kulimfanya Mungu kuhisi mpweke na mwenye upungufu. Katika hali ya kukata tamaa—na, yaweza kusemekana, kwa nadhari—Mungu alifanya kitu cha kiasili sana: Mungu aliuweka mkono Wake kwenye moyo wake na kutamka ahadi ya zawadi kwa Ibrahimu kwake Yeye Mwenyewe, na kutokana na haya binadamu akamsikia Mungu akisema “Nimeapa kwa nafsi Yangu.” Kupitia vitendo vya Mungu, unaweza kujifikiria wewe mwenyewe. Unapoweka mkono wako juu ya moyo wako, na kujizungumzia, unalo wazo wazi kuhusu kile unachosema? Je, mwelekeo wako ni wa uaminifu? Unaongea waziwazi, kwa kutumia moyo wako? Hivyo, tunaona hapa kwamba wakati Mungu alipomzungumzia Ibrahimu, Alikuwa mwenye bidii na wa ukweli.
Wakati huohuo alipokuwa Akiongea naye Ibrahimu na Akimbariki, Mungu alikuwa pia Akijizungumzia Mwenyewe. Alikuwa Akijiambia: Nitambariki Ibrahimu na kuuzidisha uzao wake kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani, kwa sababu alitii maneno Yangu na ndiye Niliyemchagua. Wakati Mungu aliposema “Nimeapa kwa nafsi Yangu,” Mungu Aliamua kwamba ndani ya Ibrahimu Angezalisha wateule wa Israeli , na baadaye Angewaongoza watu hawa kusonga mbele sambamba na kazi Yake. Yaani, Mungu angekifanya kizazi cha Ibrahimu kufanya kazi ya usimamizi wa Mungu, na kazi ya Mungu na ile iliyoonyeshwa na Mungu ingeanza na Ibrahimu, na kuendelea katika vizazi vya Ibrahimu, na hivyo kuthamini tamanio la Mungu la kuokoa binadamu. Unasemaje, hiki si kitu kilichobarikiwa? Kwa binadamu, hakuna baraka kubwa zaidi kuliko hii; hii, inaweza kusemekana, ndiyo baraka kubwa zaidi. Baraka aliyopata Ibrahimu haikuwa kuzidishwa kwa uzao wake, lakini ilikuwa Mungu kutimiza usimamizi Wake, agizo Lake na kazi Yake kwa vizazi vya Ibrahimu. Hii inamaanisha kwamba baraka alizopata Ibrahimu hazikuwa za muda, lakini ziliendelea kwa kadri mpango wa usimamizi wa Mungu ulipoendelea. Wakati Mungu alipoongea, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, tayari Alikuwa ameamua. Je, mchakato wa uamuzi huu ulikuwa kweli? Ulikuwa halisi? Mungu aliamua kwamba, kuanzia hapo kuendelea, jitihada Zake, gharama Aliyolipia, kile Anacho na alicho, kila kitu Chake, na hata maisha Yake yangekabidhiwa Ibrahimu na vizazi vya Ibrahimu. Na ndivyo pia Mungu alivyoamua kwamba, kuanzia kwenye kundi hili la watu, Angeonyesha vitendo Vyake, na kumruhusu binadamu kuiona hekima, mamlaka na nguvu Yake.

Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni